Saturday 21st, December 2024
@Mwanga
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anategemea kutembelea Wilayani Mwanga hapo kesho tarehe 24.09.2021. Katika ziara yake hiyo, Mhe. Majaliwa atatembelea na kukagua mradi mkubwa wa maji wa Mwanga - Same - Korogwe.
Baada ya kutembelea na kukagua mradi huo, Mhe. Waziri Mkuu ataongea na wananchi wa Mwanga katika kijiji cha Njiapanda Kirya kuanzia majira ya saa nne kamili asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya anawakaribisha wananchi wote waweze kumpokea Waziri Mkuu na kuweza kuhudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa