HALMASHAURI YA WILYA YA MWANGA
RASIMU YA WILAYA YA MWANGA
UTANGULIZI.
UTAWALA .
Wilaya ya Mwanga ilianzishwa mwaka 1979 na ni mojawapo kati ya Wilaya sita (6) za Mkoa wa Kilimanjaro. Kiutawala Wilaya ya Mwanga ina Tarafa 5 ( Kuna Tarafa moja mpya ya Kindoroko ambayo haijaanzishwa rasmi, ikianzishwa Wilaya itakuwa na Tarafa 6). Wilaya ina Kata 20, Vijiji 72 , Mji Mdogo wa Mwanga na kuna jumla ya Votongoji 273. Kati ya Vitongoji 273 Vitongoji 12 viko katika Mji Mdogo wa Mwanga na Vitongoji 261 viko katika Vijijini 72 vya Wilaya..
MIPAKA YA WILAYA.
Wilaya iko kati ya Nyuzi 30 25’’ na Nyuzi 30 55’’ Kusini mwa Ikweta, na iko kati ya 370 25’’ na Nyuzi 370 58’’ Mashariki mwa Mstari wa ’’Greenwhich’’.Wilaya ya Mwanga imepakana na Wilaya ya Moshi kwa upande wa Kaskazini, nchi jirani ya Kenya upande wa Mashariki, Wilaya ya Same upande wa Kusini na Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara upande wa Magharibi.
Eneo la Wilaya na Mwinuko wa Nchi.
Wilaya in ukubwa wa Kilometa za mraba 2,641 ,kati ya hizo eneo la Kilometa za mraba 2,558.6 ni la Nchi kavu na zilizobakia Kilometa za mraba 82.4 ni za maji ya Nyumba ya Mungu ( Km2 56) na Ziwa Jipe (Km2 26.4 ). Wilaya iko kati ya Mita 700 -2,212 juu ya usawa wa Bahari.
1.4 .Hali ya Hewa
Hali ya hewa wilayani kwa asilimia kubwa ni ya ukame. Kuna misimu miwili ya mvua, Vuli ambayo huanza mwezi wa Octoba hadi mwezi Disemba na Masika ambayo huanza mwezi Machi hadi Juni. Wilaya huwa na Upepo mkali na mkavu unaovuma tokea upande wa Mashariki mwa Wilaya kuelekea Magharibi. Kiwango cha joto huwa ni kati ya nyuzi joto 140 C kwenye mwezi Juni na Julai na miezi mingine huwa ni nyuzi joto 320 C . Wilaya ina Kanda 2 Kuu za Kilimo , Kanda ya Nyanda za Chini Mashariki na Chini Magharibi na Nyanda za Juu. Nyanda za Chini kiwango cha mvua kwa mwaka huwa kati ya 400mm- 600mm. na Nyanda ya Juu kiwango cha mvua kwa mwaka huwa kati ya 800mm- 1,200mm.
IDADI YA WATU.
Muhtasari wa Idadi ya Watu –Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi Toka mwaka 1978-2012.
Mwaka
|
Idadi ya Watu |
Ongezeko |
Asilimia (%) ya Ongezeko |
Idadi ya Kaya |
||
Wanaume |
Wanawake |
Jumla. |
||||
1978
|
35,621 |
38,909 |
74,530 |
- |
- |
13,551 |
1988
|
46,362 |
50,642 |
97,004 |
22,474 |
30.15 |
17,487 |
2002
|
55,327 |
59,818 |
115,145 |
18,141 |
18.70 |
24,326 |
2012
|
63,199 |
68,243 |
131,442 |
16,297 |
14.15 |
29,875 |
HUDUMA ZA KIUCHUMI.
Asilimia 85 ya wananchi wanaishi vijijini. Uchumi wa wilaya unategemea sana kilimo, ufugaji, uvuvi na sehemu ndogo wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo. Mazao makuu ya biashara yanayolimwa ni Kahawa,na Mkonge . Mazao ya chakula ni Mahindi, Maharage, Ndizi, Mihogo, Viazi vitamu na Mpunga.
2.1. Kilimo
Wilaya ya Mwanga ni wilaya ya kilimo na ufugaji na kwa kiasi kidogo uvuvi na biashara. Asilimia 85 ya Wananchi wa Mwanga wanaishi vijijini kwa kutegemea zaidi kilimo na ufugaji.Eneo linalofaa kwa kilimo ni ha 44,300, kati ya hizo hekta 7,409 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Jumla ya eneo linalolimwa na kumwagiliwa maji ni hekta 3,648, kati ya hizo hekta 2,230 humwagiliwa kwa sikimu za umwagiliaji zilizopo kati ya eneo la hekta 5,280 na hekta 1,418 humwagiliwa na Ndiva kati ya eneo la hekta 2,209. Hekta 36,891 zinategemea kilimo cha maji ya mvua.
2.5 Mifugo
Ufugaji unakwenda sambamba na kilimo kwani unachangia Wananchi kuinua kipato chao. Wapo zaidi ya ng’ombe 51,010 wa kisasa wakiwa 12,260, mbuzi 36,449 wa kisasa wakiwa 410, kondoo 22,240, nguruwe 497, punda 4,943, sungura 196, kuku 98,726, bata 11,901 na ngamia 6. Yapo malambo 9, majosho 13 na Vituo vya mifugo 9 kwa ajili ya kuboreshaufu.
2.6 Maliasili na Mazingira
.
Jina la Msitu |
Aina ya Msitu |
Mahali Ulipo/Vijiji |
Ukubwa-Ha. |
Hadhi ya Msitu |
Mramba
|
Msitu wa Asili
|
Kifaru; Kisangiro and M
Kwanyange |
3,355 |
Msitu wa Hifadhi.
|
Kirongwe
|
Msitu wa Asili
|
Kiverenge; Ngullu; and Sofe.
|
1,758.4 |
Msitu wa Hifadhi
|
Kindoroko
|
Msitu wa Asili
|
Ngujini; Chanjale; Sofe; Ndorwe; Chomvu and Kilomeni.
|
885 |
Msitu wa Hifadhi
|
Minja
|
Msitu wa Asili
|
Vuchama Ngofi
|
520 |
Msitu wa Hifadhi
|
Kamwala 1
|
Msitu wa Asili
|
Vuchama Ndambwe; Mfinga; Mkuu; Shighatini ; Kighale; and Kirongaya.
|
119.25 |
Msitu wa Hifadhi
|
Kamwala 11
|
Msitu wa Asili
|
Songoa and Ngujini.
|
292 |
Msitu wa Hifadhi.
|
Kileo
|
Msitu wa Asili
|
Kileo
|
191 |
Msitu wa Hifadhi
|
Mbachi
|
Msitu wa Asili
|
Vuchama Ngofi
|
97.4 |
Msitu wa Hifadhi
|
Mbochiro
|
Msitu wa Asili
|
Kifaru na Kisangiro.
|
588 |
Msitu wa Hifadhi
|
Total
|
7,806.05 |
|
2.8 Miundombinu/Barabara.
Wilaya ya Mwanga pamoja na kuwa na Barabara kuu ya lami yenye urefu wa km 63.5, reli km. 50 kutoka Dar es Salaam kwenda Kaskazini pamoja na nchi jirani. Wilaya ina jumla ya Barabara zisizo za Lami zenye jumla ya kilometa 744.8 , kati ya hizo Kilometa 7.5 ni za Lami, 294 ni za changarawe na kilometa 443.3 ni za udongo. Wakala wa Barabara (Tan Roads) wanahudumia km 191 na Wilaya inahudumia km. 609.8
2.9 Reli.
Kuna Reli inayopita Wilayani Mwanga yenye urefu wa kilometa 55 inayotoka Moshi kuelekea Tanga na Dar-es- Salaam. Kwa sasa hivi Reli haitumiki kwa kusafirisha abiria wala mizigo kutokana na kuwepo kwa vyombo vingi vya usafiri wa abiria na mizigo na vinvyochukua muda mfupi kwenda sehemu fulani ukilinganisha na treni, hivyo wasafiri na wasafirishaji mizigo hutumia usafiri wa barabara na kufanya usafiri wa treni kukosa abiria na mizigo.
2.10 Ushirika
Katika suala la kupambana na umaskini, wilaya imeweka nguvu kubwa katika kuanzisha na kuimarisha vyama vya akiba na mikopo (SACCOs). Wilaya kwa sasa ina SACCOS 21 zenye wanachama 4,963 ambao wamechangia hisa zenye thamani ya Tsh. 76,713,000/-, akiba Tsh. 278,157,000/- na amana za Tsh. 23,706,400/-..Katika kuendeleza miradi yao ya kiuchumi wanachama wa SACCOs wameweza kukopa kupitia vyama hivyo, jumla ya Tsh. 1,049,597,500/- na tayari wamesha rejesha Tsh. 1,098,812,600/-. Kiasi kilichobakia mikononi mwa wanachama ni Tsh. 310,784,900/-. Hata hivyo mahitaji bado ni makubwa zaidi.
2.11 Madini /Viwanda.
Wilaya ya Mwanga ina Kiwanda kimoja kikubwa cha Kilimanjari- Bio-Chem kilichopo kijiji cha Kifaru kinachotengeneza bidhaa za ‘’Spirit ‘’( 96 % Ethanol) tokana na Mollases na kimeajiri Watumishi 130 kwa sasa. Wilaya pamoja na kuwa na aina ya madini , haina Viwanda vya uchimbaji madini ya aina yoyote kwa hivi sasa kinachofanya kazi.Kuna madini ya Shaba kwa kiwango kidogo na wachimbaji waliopo ni wadogo wadogo na kiwango cha uzalishaji hakijajulikana. Pia kuna madini aina ya Jasi ambayo hayajaanza kuchimbwa na kiwango kilichopo bado hakijulikani. Kuna jumla ya Mashine za kukoboa na kusaga 73 na viwanda vidogo vodogo vya useremala na uchomaji vyuma 23 ambavyo vinatoa ajira kwa watu karibú 3,000.
2.12 Uvuvi.
Uvuvi ni shughuli muhimu inayowapatia mapato wakazi wanaokaa kandokando ya Bwawa la Nyumba ya Mungu , wastani wa Kilo 476.48 huvuliwa kwa mwaka katika Bwawa hilo zenye thamani ya Tshs. 1,511,330,200. Kuna jumla ya Wavuvi 660 na mitumbwi midogo ( Canoes) 378 .
2.13 Ufugaji Nyuki.
Shughuli za ufugaji Nyuki na uzalishaji wa Asali na Nta ni kidogo sana katika Wilaya ya Mwanga kuna Mizinga ya asili 2,500 na ya Kisasa 135 inayozalisha wastani wa Kilo 720 kwa mwaka yenye thamani ya Tshs.5,760,000.
2.14 Biashara
Wilaya ina idadi ya biashara zifuatazo:- Baa 55, ‘’Grocery’’ 18, Maduka ya rejareja 1,523, ‘’Viosk’’ 45, Bucha 41, Mikahawa 14, ‘’Garage’’ 2,Maduka ya rejareja na jumla 5, Hotel 3- Kindoroko Mountain Lodge- Kisangara, Mhako Hotel- Usangi na Anjela Inn Hotel Mwanga Mjini. Motel 2-Mwanga Mjini, Nyumba za kulala wageni 16, na kuna Vituo vya Mafuta 5 vinavyofanya kazi, Mwanga Mjini 2, Kifaru 1, Kisangara 1 na Mgagao 1.
2.15 Nyumba za kufikia Wageni na Viongozi.
Wilaya ina ‘’Rest House’’ moja ya kufikia Viongozi Wakuu wa Serikali ya Serikali Kuu na nyingine moja ya Halmashauri.
3.0 HUDUMA ZA JAMII
3.1 Rasilimali Za Maji
Wilaya ya Mwanga ina Ziwa Jipe ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 26.4 na likiwa limekaa katika mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania na Bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo lina ukubwa wa kilometa za mraba 140.
Vyanzo vikuu vya Maji kwa Vijijini ni Chemu chemu za asili, Ziwa Jipe, Bwawa la Nyumba ya Mungu na Mto Pangani.
3.2 ELIMU.
3.2.2 Elimu ya msingi
Uandikaishaji katika Shule za Msingi mwaka 2012.
Wilaya ina Shule za Msingi 113, kati ya hizo 109 ni za Serikali na 4 ni za watu binafsi Kuna jumla ya wanafunzi 30,005 kati yao 15,209 wavulana na wasichana 14,796. katika Shule za Serikali 29,825, Wavulana 15,115 na Wasichana 14,710. Wastani wa mahudhurio shuleni ni asilimia 98.01 . Kati Shule 113 za Msingi kuna Shule maalum 18 za walemavu kama ifuatavyo:- Shule ya Elimu Maalum kwa Viziwi 1 (Mwanga), mchanganyiko kitengo cha Viziwi 1- Mramba, na Elimu Jumuishi 16.
3.2.3 Elimu ya Sekondari.
Shule za sekondari zipo 41, kati ya hizo 25 ni za Serikali na 16 ni za binafsi, kati ya hizo Shule zenye Kidato cha I-VI ni 13 , Shule 5 zikiwa ni za Serikali na 8 za binafsi. Pia kuna Vyuo 3 vya Ufundi Stadi na Chuo kimoja cha binafsi cha Ualimu
3.2.4 Vyuo vya Elimu ya Ufundi (VETA).
Kuna Vyuo vya VETA 6 , 3 ni vya Serikali na 3 ni vya binafsi.
3.3 AFYA
Vituo vya Tiba Vilivyopo.
Aina/Mmiliki |
Idadi |
Hospitali za Serikali
|
1 |
Hospitali za Taasisi/ Binafsi
|
0 |
Vituo vya Afya vya Umma
|
5 |
Vituo vya Afya vya Taasisi/Binafsi
|
1 |
Zahanati za Umma
|
40 |
Zahanati za Taasisi/ Binafsi
|
5 |
3.4 MAENDELEO YA JAMII.
Mfuko wa Wanawake (WDF)
Mfuko huu uko rasmi kwa ajili ya kuwakopesha wanawake ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi hatimaye kujikwamua na janga la umaskini.
Vikundi mbalimbali
Wilaya ya Mwanga ina vikundi (CBOS) 390, Asasi za kijamii 5.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa