• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

Fursa za Kilimo

FURSA YA UWEKEZAJI KWENYE KILIMO

Sehemu kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Mwanga, kazi wanayo jishughulisha nayo ni kilimo, ufugaji na uvuvi. Kahawa na zao la ndizi zinalimwa maeneo ya milimani ambako mvua huwa ni za uhakika zaidi kuliko maeneo ya tambarare. Pia maeneo ya milimani wanatumia maji ya umwagiliaji ambayo huwa yanafahamika zaidi kama maji ya ndiva. Kwa upande wa maeneo ya tambarare ya mashariki, kaskazini na magharibi mvua huwa ni kidogo sana hivyo maeneo haya kilimo cha umwagiliaji ndicho kinacho limwa zaidi. Maeneo haya yanalimwa zaidi zao la mahindi, maharage, vitunguu na mpunga.

Zao kubwa linalo limwa Wilayani Mwanga ni Mahindi, fiwi, mpunga, ndizi, kahawa, matunda na mbogamboga. Kwa wastani kila mwaka uzalishaji wa mahindi ni tani 6,500, mpunga tani 350, maharage tani 1,100, maparachichi tani 3,000, ndizi tani 15,000 na kahawa ni tani 90.

Wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali wanakaribishwa Wilayani Mwanga kutumia fursa na rasili mali ya ardhi iliyopo ili waweze kuwekeza kwenye kilimo kwani ardhi ipo ya kutosha.

Maeneo ambayo yanatoa fursa ya uwekezaji wa kilimo ni pamoja na;

Kilimo cha umwagiliaji Kirya, Kileo na Kivulini. Kuna jumla ya hekta 900 za umwagiliaji kwenye Kata ya Kirya ambapo, hadi sasa hekta 150 tu ndizo ambazo zinatumika. Wawekezaji wanakaribishwa kuja kuendeleza hekta zilizo baki ambazo zina rutuba nzuri na hali ya hewa nzuri inayo ruhusu kilimo cha Umwagiliaji kwenye eneo hili. Eneo lingine ambalo linafaa sana kwa kilimo cha umwagiliaji ni Kijiji cha Kileo chenye jumla ya hekta 2,400 ambazo zinafaa kulimwa kwa kipindi chote cha mwaka. Kijiji cha kivulini kina jumla ya hekta 1,050 ambapo, hekta zinazotumika kwa kilimo ni 400 tu. Tarafa ya Jipe Ndea nayo ni miongoni mwa maeneo yenye ardhi ya kutosha inayo faa kwa kilimo. Maeneo yote haya yanafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama alizeti, mtama, uwele, miwa, mahindi, maharage, fiwi/ngwara, korosho, mbogamboga, matunda na mpunga kwa maeneo ya Kirya na Kileo.

Maeneo ya kujenga viwanda vya kusindika mazao. Kutokana na uwepo wa maeneo mengi ya kulima mazao ya aina tofauti, Wilaya inawakaribisha wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya usindikaji wa mazao kama kahawa, alizeti, mpunga,mahindi na mazao ya matunda na mbogamboga.

Kuanzisha maduka ya pembejeo za kilimo. Mazao mengi yanapokuwa shambani yanahitaji viwatilifu ili kuuwa wadudu wanao shambulia mazao. Pia wakulima wanahitaji pembejeo mbalimbali za kutumia shambani kama mbolea na mbegu. Kwasababu hii wakulima wanapata shida ya kupata pembejeo kwa wakati kutokana na kufuata madawa kwenye maduka yaliyoko mbali na eneo la kilimo. Hivyo hii ni fursa nzuri kwa wazawa na wasio wazawa kuja kuwekeza Mwanga na kuweza kuanzisha maduka ya pembejeo za kilimo ili kuwarahisishia wakulima kwenye huduma ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo.

Fursa nyingine iliyopo kwenye sekta ya kilimo ni pamoja na uwepo wa maeneo ya kuchimba mabwawa ya kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji pamoja na ujenzi wa masoko ya mazao mbalimbali kwenye Kata za, Kileo, Mwanga, Mgagao na Lembeni.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa