Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Kiseo Nzowa mapema leo septemba 25, 2025 amefanya ziara ya kukagua miradi 4 ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na kueleza kuridhishwa kwake na namna miradi hiyo ilivyotekelezwa.
Akizungumza katika ziara hiyo Bw. Nzowa amepongeza Mkurugenzi na Timu yake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na alimuelekeza Mkurugenzi kuongeza kasi ya utekelezaji ili Miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Aidha amemtaka mhandisi wa wilaya kufanyia kazi ushauri uliotolewa na wataalamu katika ziara kwenye baadhi ya maeneo muhimu katika miradi.
Katika ziara hiyi Katibu Tawala ametembelea Miradi 4 ikiwemo Mradi wa Ukamilishaji wa ujenzi wa majengo 5 katika Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Zahanati ya toloha, ujenzi wa shule ya msingi ya Mkondo mmoja Mlevo na Ujenzi wa mabweni 2 sekondari ya Ubang’i
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa