• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

Ufugaji wa Mifugo

TAARIFA YA OPRESHENI

Mwezi Septemba 29 – 20 octoba 2017, Wilaya ilitekeleza sheria ya kuithibiti Mifugo iliyoingizwa na kuikamata jumla ya Mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria ya kuthibiti magonjwa ya wanyama ya “Veterinary Act”. Kifungu cha 43 (a) na (b)  ya mwaka 2003 na kutaifishwa na Serikali hadi kufikishwa katika mnada wa hadhara Mifugo 1,118 na iliyouzwa mnadani ni ng’ombe 1,113, punda mmoja (1) na Kondoo mmoja (1) na ng’ombe mmoja (1) alifia mnadani. Aidha, kupitia kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na ng’ombe wane (4) ilithibitishwa kuwa walikuwa wanamilikiwa na mfugaji mwenyeji ambaye alirudishiwa ng’ombe hao bila masharti yoyote.

Mnada uliendeshwa kwa kunadisha ngombe kwa mafungu ya ng’ombe ishirini ishirini kwa uwazi na ushindani. Bei ilitamkwa na mnunuzi aliyefikia bei ya juu aliuuziwa. Baada ya kuuza ng’ombe wote jumla ya TSH 238,080,000/= (milioni mia mbili thelathini na nane  na elfu themanini) zilikusanywa ikijumuisha ushuru wa soko uliolipwa kwa Halmashauri ya Mwanga kwa kuuza ng’ombe 1,065 (elfu moja na sitini na tano) na kondoo 1 (mmoja). Ambapo punda mmoja hakuuzwa kwa kukosa mnununzi. Pesa zinajumuisha malipo yafuatayo:

  1. Mauzo ya mifugo sh. 231,024,500/=
  2. Vibali vya usafirishaji nje na ndani ya mkoa sh, 1,795,500/=
  3. Ushuru wa soko sh. 5,260,000/=

Ushuru wa soko ulilipwa kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Own source akaunti namba 40210000551 iliyoko NMB Mwanga.

1.4 UPIGAJI CHAPA KWA MIFUGO (NG’OMBE)

Kwa kuzingatia agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu mnamo tarehe 15/06/2017 mkoani Dododma kwa maafisa Mifugo wote nchini linalohusu utambuzi na upigaji chapa wa mifugo ili kupanga matumizi bora ya ardhi na kumaliza migogoro ya watumiaji ardhi yakiwemo makundi ya wakulima na wafugaji.

Zoezi la upigaji chapa ng’ombe limeanza kutekelezwa tarehe 30/10/2017 katika Kata ya Kirya ambapo jumla ya ng’ombe 3,570 wamepigwa chapa.

Idadi ya ng’ombe waliopigwa chapa

KATA
KIJIJI
KITUO CHA UPIGAJI CHAPA
TAREHE
IDADI YA NG’OMBE SAJILIWA
Kirya
Kirya
Kirya
30/10/2017
216
01/11/2017
371
02/11/2017
202
Mangulai
04/11/2017
753
Mangulai
06/11/2017
929
Stafu
07/11/2017
482
Njiapanda
S/moyo
22/11/2017
617
JUMLA
3,570

1.5 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE

Changamoto

Baadhi ya viongozi hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa wataalam kuhakikisha wafugaji wote wanaleta mifugo yao kwa wakati muafaka ili kukamilisha zoezi la upigaji chapa mapema.

Mvua za vuli zilizoanza kunyesha zimekuwa zikikwamisha zoezi la upigaji chapa.

Wafugaji kuwapangia wataalam muda wa kufanya kazi kuwa ni kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 4:00 asubuhi kwa madai kuwa wanataka mifugo yao ikachunge.

Vyuma vya chapa kupinda.

Mifugo mingi kutokuwepo katika vijiji vyao mala baada ya kuhama kwenda kutafuta maji na malisho.

Namna ya kuzikabili

Sheria kali ikiwemo kutozwa faini isiyozidi milioni mbili (2,000,000/=) zitachukuliwa dhidi yao wote watakaokaidi zoezi hili nyeti na kuchelewesha kufanikisha zoezi la upigaji chapa wakati na baada ya zoezi kukamilika 30 Desemba 2017.

Halmashauri iliamuru kazi kufanyika kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni kwa siku mbili tu na baada ya hapo wataalam kuhamia kituo kingine.

Halmashauri imechukua hatua za haraka kwa kuandaa vyuma imara na kazi kuendelea

Wafugaji wameshauriwa kurudisha mifugo yao kwakuwa mvua zimeanza kunyesha na majani kuchipua.

1.6 MIKAKATI

· Kutoa elimu kwa wafugaji wote wa Kata zote 20 za Wilaya ya Mwanga, ambapo mpaka sasa Kata za Kirya, Lang’ata, Kileo, Lembeni, Mgagao, Toloha, Mwanga, Kivisini, Jipe, Kigonigoni na Kwakoa kumeshafanyika mikutano ya kutoa elimu na uhamasishaji wa kupiga chapa.

·Kuzuia mifugo isiyo na chapa kuuzwa mnadani, kusafirishwa na kupelekwa machinjioni mala baada ya ratiba ya upigaji chapa mifugo kukamilika.

·Mala baada ya kumaliza kupiga chapa kwa kata na kijiji, timu ya wataalam inahamia Kata na vijiji vingine.

·Timu ya wataalam inapomaliza kupiga chapa eneo moja, Afisa mtendaji wa Kata husika kwa kushirikiana na mtaalam wa Mifugo wa Kata na viongozi wengine watafuatilia Mifugo yote ambayo haikupigwa chapa na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi kwa hatua zaidi za kisheria.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa