• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

DED MWANGA ATOA MAELEKEZO MAZITO KWA WATUMISHI, ASEMA “KILA MTUMISHI ASIMAME KWENYE NAFASI YAKE”

Posted on: October 5th, 2021

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Mwajuma A. Nasombe leo amekutana na watumishi wa idara mbalimbali kutoka kwenye ngazi ya Kata. Watumishi aliokutana nao ni Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Wataalamu wa Afya, Maafisa Mifugo, Maafisa Kilimo, Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa shule na Walimu Wakuu.

Mkurugenzi amekutana na watumishi hao katika ukumbi wa Mwanga Sekondari ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na kupata wasaa wa kuwakumbusha na kuwaelekeza juu ya masuala mbalimbali ya utendaji kazi za Serikali za kila siku.

Akiwa katika kuwakumbusha na kuwaelekeza juu ya majukumu yao, Mkurugenzi amesema kuwa, watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mambo makuu matatu ambayo ni Sera, Taratibu na Kanuni (STK). Amewakumbusha kuwa, vyeo walivyonavyo ni dhamana hivyo wanapaswa kuvifanyia kazi kwa usahihi kwa manufaa ya serikali na wananchi wake na siyo kwa maslahi binafsi. “Mkae mkijua kuwa, vyeo mlivyonavyo siyo kwamba nyie ni bora kuliko wengine, bali hicho cheo ni dhamana, na wala usiwanyanyase unaowaongoza, bali waelekeze”, alisema Mkurugenzi.

Aidha katika maelekezo yake, hakuacha kuzungumzia suala la watendaji wa serikali kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi na kutatua kero zinazo ikabili jamii. Amewataka watumishi hao kuhakikisha kuwa, wanafanya kazi kwa uwadilifu na uwajibikaji. Ameendelea kusema kuwa, baadhi ya watendaji wa vijiji wamekuwa kama miungu watu, hawataki kutembelea wananchi na kuatatua kero zao. Amesisitiza kuwa, haipendezi kuona mambo madogo yanayoweza kutatuliwa katika ngazi za chini yanafika ofisini kwake ama kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Masuala kama hayo yatatuliwe katika ngazi za chini na yakishindikana kabisa, ndipo yafike katika ngazi za juu, amesema Mkurugenzi.

Sambamba na hayo, pia hakuacha kuzungumzia kukerwa na baadhi ya watendaji wa serikali kuzembea suala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri. Amesema kuwa, kuna baadhi ya watumishi wa Halmashauri wamepewa kazi ya kusimamia na kukusanya mapato ya Serikali lakini hawafanyi kazi hiyo kwa ufasaha hata wakati mwingine wanafikia hatua ya kuhujumu juhudi za ukusanyaji wa mapato. Mkurugenzi amesema kwamba, watumishi wa namna hii hata wanyamazia na atawachukulia hatua za kinidhamu pale atakapobaini kuna uzembe katika suala la kukusanya mapato ya Serikali.

Akizungumza juu ya miradi mbalimbali ya Serikali amesema kuwa, kuanzia sasa ameamua vifaa vyote vya ujenzi vitakavyohitajika kwa ajili ya kujenga miradi inayoendelea hapa Wilayani, vitaagizwa kiwandani na vifaa vichache ambavyo vitakuwa havipatikani kiwandani vitaagizwa kutoka kwenye maduka ya kawaida. Lengo kuu likiwa ni kuokoa gharama kubwa zinazotumika katika kununua vifaa vya ujenzi kutoka kwenye maduka ya kawaida. Amesisitiza kuwa, vifaa kama saruji, chokaa, mabati, nondo, mbao na rangi vitakuwa vinaagizwa kutoka kiwandani ili kuokoa gharama za ujenzi.

Katika mazungumzo yake, Mkurugenzi amewasisitiza watumishi wote wa Halmashauri ya Mwanga kuhakikisha kuwa wanachanjwa chanjo ya UVIKO – 19. Amesema kuwa, watumishi wamepewa dhamana ya kuaminiwa na serikali na ndiyo maana wao ni watumishi wa umma, hivyo wanapaswa kuwa mfano bora katika kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanikiwa kwa wao kuchanjwa na kuihamasisha jamii nayo ili iweze kupata chanjo. “Chanjo hii ni salama, na ndio maana mimi Mkurugenzi wenu pamoja na DC wenu tumechanja na hatujapata madhara yeyote, hivyo kila mtumishi ahakikishe anapata chanjo hii kwa ajili ya afya yake na jamii yake”, Amesema Mkurugenzi. 

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa