• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA CHANZO MUHIMU CHA MAPATO YA HALMASHAURI

Posted on: October 13th, 2018

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri,  jana imetembelea Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa lengo la kubaini na kuweka mikakati mizuri ya kuweza kuinua kiwango cha makusanyo ya mapato yatokanayo na uvuvi wa samaki na mazao yatokanayo na samaki..

Kamati hiyo iliyo ongozwa na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri,  Bi.Theresia P. Msuya, iliweza kukutana na vikundi vinavyohusika na uangalizi na uzuiaji wa uvuvi haramu (BMU - Beach Management Unit) na kupokea changamoto mbalimbali ambazo BMU wanakutana nazo. Vikundi hivyo vilieleza kuwa, miongoni mwa changamoto walizonazo ni pamoja na kina cha maji kupungua kwa haraka kutokana na uhitaji wa maji ya umwagiliaji, nyavu kuibiwa mara kwa mara, kuonewa na vyombo vya dola, ufungaji wa bwawa mara kwa mara, ushuru mkubwa wa samaki, uwepo wa wanyama aina ya viboko ziwani na uhaba wa wataalam wa uvuvi.

Pamoja na changamoto hizo, Mhe. Theresia akiongea na wavuvi hao kwa nyakati tofauti, alisema, suala la kufunga bwawa mara kwa mara lipo mikononi mwa wavuvi wenyewe, endapo wataacha kutumia nyavu haramu na kuvua samaki wadogo, bwawa haliwezi kufungwa, ila wakitumia nyavu haramu bwawa litafungwa.

Mhe. Theresia aliendelea kusisitiza kuwa, ni jukumu la kila mvuvi kuhakikisha anazuia uvuvi haramu kwa kuachana na kutumia makokoro ili wavuvi wapate kipato na Serikali ipate kipato. Pia ameagiza kuwa, kila mwenye mtumbwi ahakikishe ameusajili kwani kuna baadhi ya mitumbwi haina nambaza usajili.

Ameongeza kuwa, Halmashauri ina fedha nyingi za kukopesha vijana, wanawake na walemavu. Hivyo anatoa wito kwa wavuvi, kujiunga kwenye vikundi vidogovidogo ili waweze kuomba mkopo na uwasaidie kwenye shughuli zao za uvuvi.

Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ni miongoni mwa Halmashauri zilizofanya vizuri sana kwenye ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2017/18. Kwa mwaka 2018/19, Halmashauri imejipanga kuhakikisha kuwa, inaendelea kufanya vizuri zaidi kwenye ukusanyaji wa mapato na ndio maana kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara yake kwenye chanzo hiki cha mapato yatokanayo na samaki na mazao yake, kwa lengo la kujifunza, kubaini na hatimaye kutoa ushauri kwa wataalam juu ya namna bora na nzuri ya kukusanya mapato ya Halmashauri.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa