• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

MIFUGO ZAIDI YA 376,205 KUVALISHWA HERENI WILAYANI MWANGA; ZOEZI LAZINDULIWA NA DC. MWAIPAYA

Posted on: March 14th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya, leo amezindua zoezi la kuvalisha hereni mifugo ya wafugaji Wilayani Mwanga. Uzinduzi wa zoezi hilo umefanyika katika Kijiji  cha Kwakihindi Kata ya Kigonigoni na kushuhudiwa na jamii ya wafugaji wa kimasai pamoja na viongozi wa wafugaji wa wilaya ya Mwanga.

Katika uzinduzi huo Mhe. Mkuu wa Wilaya amewaasa wafugaji wote wa Wilaya ya Mwanga kuhakikisha kuwa mifugo yao inavalishwa hereni kwa mujibu wa sheria. “Zoezi hili siyo la kwangu wala siyo la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, bali ni zoezi ambalo lipo kisheria na Serikali inalitambua kwa mujibu wa sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010”, alisema Mkuu wa Wilaya. Katika maelekezo yake amewataka viongozi wa wafugaji wa wilaya kuhakikisha zoezi hili linakamilika tarehe 30/03/2022 na endapo matokeo chanya hayataonekana, viongozi wa wafugaji husika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Ameendelea kusema, haoni sababu ya zoezi la kuvalisha mifugo hereni likisuasua wakati wafugaji wote walishapatiwa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hili na viongozi wa wafugaji kitaifa walishiriki kikamilifu katika kuwaelimisha wafugaji hao.

Akisoma taarifa ya zoezi la uvalishaji mifugo hereni mbele ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Mifugo Ndg. Emil Mkemwa amesema kwamba, zoezi la uvishaji mifugo hereni lilianza toka tarehe 14/02.2022. Halmasahuri inatarajia kuvalisha hereni Zaidi ya ng’ombe 134,799, mbuzi 159,050, kondoo 80,699 na punda 1,657. Katika taarifa yake hiyo amesema, mpaka kufikia tarehe 12/03/2022 jumla ya mifugo 7,879 (ng’ombe 3,869, mbuzi na kondoo 4,010) imeshavishwa hereni katika kata tatu ambazo ni Toloha, Mgagao na Kigonigoni.

Zoezi la kuvisha mifugo hereni lina faida kubwa kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla. Faida zitokanazo na uvishwaji wa hereni ni pamoja na Taifa kupata takwimu sahihi ya mifugo iliyopo, kukabiliana na magonjwa ya mlipuko (chanjo), kurahisisha biashara ya mifugo ndani na nje ya nchi, uthibiti wa wizi wa mifugo na upatikanaji wa  mikopo pamoja na bima ya mifugo.  

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa