• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

NAIBU WAZIRI APONGEZA UONGOZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MWANGA, ATOA USHAURI KUHUSU ZAHANATI ZA LEMBENI NA KILEO

Posted on: February 13th, 2020

Jana tarehe 12 Februari, 2020, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dr. Faustine Ndugulile alifanya ziara ya kikazi Wilayani Mwanga na kuweza kutembelea Hospitali ya Wilaya Usangi na baadae kutembelea zahanati za Lembeni na Kileo.

Katika ziara yake hiyo, Dr. Ndugulile alifurahishwa kwa namna huduma mbalimbali zinavyoendeshwa katika hospitali ya wilaya, mathalani namna malipo yanavyofanyika, utunzaji wa kumbukumbu na uwepo wa madawa hospitalini hapo. Waziri hakuacha kuweka wazi namna alivyofurahishwa na njia nzuri ya ukusanyaji wa mapato kielekroniki ambapo njia hii imepelea mapato kuwa makubwa na kutoruhusu mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali. Mapato ya hospitali hiyo ambayo yanatokana na malipo ya papo kwa papo, NHIF  na CHF kwa sasa yamefikia wastani wa milioni kumi kwa mwezi na yanategemea kuongezeka.

Aidha, Mhe. Waziri aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali imetoa milioni mia nne kwa ajili ya hospitali hiyo na ametoa maelekezo kuwa, fedha hizo zifanye kazi ambayo ni ya kuonekana na inayoendana na thamani halisi ya fedha hizo.

Akielezea mikakati ya kuzitumia fedha hizo, Mganga Mfawadhi wa hospitali Bi. Upendo I. Shuma alisema, uongozi umeshakaa na kuona kwamba, kuna umuhimu wa kujenga majengo mapya matatu ambayo ni jengo la maabara, upasuaji na jengo la mama na mtoto. Mhe. Waziri aliridhishwa na mipango mizuri ya namna fedha hizo zitakavyotumika na kuongezea kwamba, zitumike vizuri na kama zitabaki, ziweze kufanya jambo lingine la kuonekana hospitalini hapo.

Sambamba na hayo, Dr. Ndugulile alitoa ushauri kuhusu zahanati za Lembeni na Kileo na kusema kwamba, zahanati hizi zinapaswa zikamilike kwa haraka ili wananchi waendelee kunufaika na huduma nzuri za matibabu zitakazokuwa zinatolewa katika zahanati hizo. Akiwa katika zahanati ya Lembeni, Mhe. Waziri alichangia mifuko 50 ya saruji ikiwa ni hatua ya kuunga mkono umaliziaji wa jengo jipya la zahanati hiyo. Katika zahanati ya Kileo, aliagiza kwamba, ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa wakae na kuweka mikakati mizuri ya namna ya kuendeleza mradi mpya wa jengo la zahanati ya Kileo. Pia alimwagiza mganga mfawidhi wa kituo hicho kuhakikisha kwamba, sehemu ya mapato yanayopatikana katika zahanati hiyo, yanafanya ukarabati mdogomdogo kwenye jengo la zahanati linalotumika kwa sasa.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa