• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

SHIRIKA LA WORLD VISION LIMETOA MSAADA WA CHAKULA SHULENI KATIKA WILAYA YA MWANGA NA SAME; MKUU WA MKOA AFURAHISHWA

Posted on: March 22nd, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Same zimepokea msaada wa chakula chenye thamani ya Tsh. 234,416,150/= kutoka kwenye shirika lisilo la Serikali la World Vision Tanzania. Akisoma hotuba yake kwa Mhe. Mgeni Rasmi, Bi. Nesserian Mollel, ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi wa shirika hilo alisema, vyakula hivyo, ambavyo ni mahindi, maharage na mafuta ya kula vitawanufaisha wanafunzi 12,809 kutoka katika shule za msingi 40 na shule 9 za sekondari zilizopo katika wilaya za Mwanga na Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

Zoezi la kuzindua, kukabidhi na kugawa chakula hicho lilifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin H. Babu jana tarehe 21 Machi, 2023 katika shule ya Msingi Mangara iliyopo Wilayani Mwanga. Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi chakula hicho kwa Wakuu wa Wilaya za Mwanga na Same, Mhe, Mkuu wa Mkoa alisema kwamba, amefurahishwa sana  anashukuru shirika la World Vision Tanzania kwa uzalendo waliounyesha kwa kutoa msaada wa chakula shuleni. Alisistiza kwamba, chakula hiki kinakwenda kuwa msaada mkubwa kwa muda wa miezi mitatu kwa wanafunzi, na hii itasaidia kuongeza mahudhurio, kupunguza utoro wa rejareja, kuongeza ufaulu na utulivu kwa wanafunzi.

Katika hotuba yake pia, Mhe. Mkuu wa Mkoa pia alizungumzia suala la malezi kwa wanafunzi, huku akiwasisitiza wazazi pamoja na jamii ya Mwanga na Same kuhakikisha kwamba, mtoto anapata malezi mazuri ili aweze kuwa na maadili mema katika jamii. Pia ametoa wito kwa viongozi wa dini kukemea tabia mbaya na ovu ambazo zimekuwa zikiibuka katika jamii na kupelekea uwepo wa mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

Wilaya ya Mwanga, siku za karibuni pia imenufaika na msaada wa vyakula kutoka taasisi mbili za kidini. Taasisi hizi ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa wanachi ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na BAKWATA.  

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa