• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

SIJARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA MGANGA MFAWIDHI NA MTUNZA STOO KATIKA KITUO CHA AFYA KISANGARA – DED MWANGA

Posted on: September 22nd, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Mwajuma A. Nasombe amesema kuwa, hajaridhishwa na utendaji kazi wa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kisangara na Mtunza stoo wa kituo hicho. Ameyasema hayo leo alipotembelea kituo hicho ikiwa ni mara yake ya pili kufika hapo baada ya kutembelea tena tarehe 17 Septemba, 2021.

Kitendo cha kutoridhishwa na utendaji wa watumishi hao, imepelekea Mkurugenzi Mtendaji kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi juu ya mapungufu ya awali yaliyobainika katika kituo hicho. Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa, tarehe 17 septemba, 2021 alifika katika kituo hicho na kubaini kuwa, kuna mambo mengi yasiyoridhisha kwenye mapokezi, utunzaji na utoaji wa dawa kwa ajili ya wagonjwa, wagonjwa kununua dawa/vifaa tiba nje wakati dawa zipo kituoni, baadhi ya dawa zikitoka stoo hazifiki katika chumba cha kutolea dawa ikiwa ni pamoja na chumba cha kutolea dawa kuwa na watoaji huduma wengi kinyume na taratibu.

Aidha, baada ya Mkurugenzi Mtendaji kubaini dosari zilizopo katika kituo hicho, tarehe 18 septemba, 2021 aliunda timu ya wataalamu sita kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi kituoni hapo ambapo, kwa uchunguzi wa awali imebainika kuwa, kuanzia mwezi julai, 2020 hadi tarehe ya ukaguzi (18/09/2021) kituo kilinunua dawa zenye thamani ya Tsh. 19,693,898.16 ambapo katika fedha hizo, dawa zenye thamani ya Tsh. 3,134,500 hazikuingizwa kwenye leja, pili, kukosekana kwa jalada la nyaraka za mapokezi ya dawa, tatu, menejimenti kutozingatia miongozo juu ya kuingiza bidhaa katika leja kabla ya kufanya matumizi na nne,  kukosekana kwa mtu sahihi juu ya utunzaji wa nyaraka za mapokezi ya kituo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwanga ambaye alifika Wilayani Mwanga mwezi Agosti, 2021, amekuwa akifanya ziara za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri kwa ajili ya kujionea namna ambavyo watumishi wanawajibika katika kutoa huduma kwa wananchi na serikali yao. Pia amekuwa akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo mingi inatekelezwa na fedha kutoka serikalini, wahisani na wananchi.  Ziara kama hizi zimekuwa na manufaa kwa Halmashauri kwani inasaidia kubaini changamoto ambazo zipo na namna ya kukabiliana nazo.

 

 

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa