• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

WANANCHI TUMIENI MSIMU HUU WA MVUA KUPANDA MAZAO; ASEMA KAIMU MKUU WA IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Posted on: March 19th, 2018

Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Ndugu Hassan M. Msuya ametoa wito kwa wananchi wa Mwanga kuhakikisha kuwa, wanatumia msimu huu wa mvua kupanda mazao kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha ili kuepukana na njaa ya baadae.

Akizungumza akiwa ofisini kwake Ndugu Mamboleo amesema, katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Mwanga hawapati uhaba wa mbegu za mahindi, alizeti na muhogo, Halmashauri kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti ya Seliani, wameweza kupata mbegu nzuri zinazohimili hali ya hewa na wananchi wanahamasishwa kufika ofisi za kilimo ili waweze kupatiwa mbegu hizo kwa bei nafuu.  Kiasi cha mbegu za mahindi zilizopokelewa ni tani 4, hadi sasa zimeshanunuliwa tani 2 ½ na zimebaki tani 1 ½. Amesema kwa sasa mtawanyiko wa mvua upo wilaya nzima ya Mwanga na atashangaa sana kuona wananchi wanaojihusisha na kilimo kama watakuwa hawazitumii mvua hizi za masika vizuri.

Sambamba na kuhakikisha kuwa  wanapanda mazao, amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanapiga dawa kwenye mashamba yao mara kwa mara kwani kuna aina mpya ya viwavijeshi ambavyo ni hatari sana kwa mazao na endapo wakulima hawatapiga dawa, basi watambue kuwa watavuna chini ya kiwango, ama wasivune kabisa. “Wananchi wabadilike kifikra kwa kuhakikisha wanapiga mazao dawa.”alisema Ndugu Msuya. Akiainisha aina ya viwatilifu vinavyofaa kwa mazao alisema wakulima watumie viwatilifu aina ya  Dasban, Duduba na Duduol sambamba na kuhakikisha shamba lenye mazao linafanyiwa usafi mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya sherehe za nanenane kwa mwaka 2018 Ndugu Msuya amesema kwa sasa Halmashauri imeshaanza maandalizi ya awali na maandalizi haya yanakwenda hatua kwa hatua. Kwa sasa Idara imeshaanza kuandaa vipando kwenye eneo la maonyesho ambalo lipo katika viwanja vya nane nane Arusha. Ifikapo tarehe za mwishoni za mwezi machi na mwezi aprili, zoezi la kushindanisha wakulima kwa ngazi ya kijiji, kata, wilaya na mkoa itakuwa imefanyika ili kupata wakulima wazuri watakaoshirikishwa kwenye maonyesho ya nane nane.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa