• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

WANANCHI WA MAMLAKA YA MJI MDOGO MWANGA WAPEWA ELIMU JUU YA RASIMU MPYA YA MKATABA WA HUDUMA YA MAJI KWA MTEJA

Posted on: March 21st, 2018

Katika kuhakikisha kuwa mwananchi wa Mji wa Mwanga anapata huduma nzuri ya maji na ya kiwango chenye tija Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanga Mjini imeandaa rasimu ya mkataba wa huduma kwa mteja, rasimu ambayo kwa hatua za awali imeshawasilishwa EWURA na sasa imeletwa kwa wananchi ili waione, waisome na kuijadili na baade irudishwe EWURA kwa hatua zaidi.

Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Ndg. Aaron Y. Mbogho ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wakati wananchi wa mji wa Mwanga wakisomewa rasimu hiyo alisema ameipitia rasimu na ameiona ni nzuri ila anaomba wananchi ambao ndio wadau wa maji waweze kuipitia na kama kuna chochote cha kuongezea basi kitatoka kwa wadau wa maji.

Akiwasilisha rasimu hiyo kwa wananchi wa mamlaka ya mji wa Mwanga, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanga Mjini Bi. Stellah Shija alisema rasimu ya mkataba huo ni nzuri kwasababu, imebeba mambo mbalimbali ambayo yatamnufaisha mteja ikiwa ni pamoja na mamlaka kujikita kwenye kuhakikisha kuwa, inatoa huduma nzuri ya maji, kusambaza matawi, kurekebisha miundombinu, kusikiliza kero za wateja, usomaji wa dira za maji, uzalishaji na usambazaji wa maji, kuzifanyia matengenezo dira za maji sambamba na kuhakikisha haki za mteja zinazingatiwa.

Akiendelea kuwasomea na kuwaelimisha wananchi wa Mji wa Mwanga juu ya rasimu hiyo, Bi. Shija alisema, rasimu inampa mteja haki ya kupewa fidia pale mamlaka ya maji itakaposhindwa kufikia malengo ya utoaji wa huduma kwa mteja na hii ni kwa mujibu wa kanuni ya mwaka 2016 ya usambazaji wa maji safi na usafi wa mazingira (ubora wa utoaji wa huduma). Akiainisha fidia hizo alisema fidia halisi zitaanzia Tsh. 10,000 na fidia ya juu itakuwa Tsh.40, 000 na hii itategemea na aina ya huduma ambayo haikutolewa kwa wakati huo.  Fidia hii itatolewa pale tu ambapo lengo la utoaji wa huduma litakuwa halikupata kutekelezwa kwa wakati.

Bi. Shija alieleza kuwa pale ambapo mamlaka ya maji itachunguza malalamiko ya mteja na kugundua kuwa kuna kasoro zimejitokeza mteja atapewa fidia ya gharama zisizo za kifedha na mteja ataombwa msamaha kwa maneno na maandishi, mteja atapewa huduma aliyostahili siku hiyo hiyo baada ya mamlaka kugundua kulikuwa na kasoro. Mteja pia anaweza kudai fidia ya fedha alizotumia kama gharama za usafiri, posta, simu au madai mengine yenye uthibitisho unaokubalika kwenye kanuni za fedha. Aidha amesisitiza kuwa fidia zote zitakazobainika na kutakiwa kulipwa hazitakuwa fedha taslim ispokuwa kwa kuweka kumbukumbu ya malipo (credit transaction) kwenye akaunti ya mteja ya malipo ya huduma ya maji safi.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa