• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

WILAYA YA MWANGA YAKAMILISHA MADARASA MAPYA KWA AJILI YA KIDATO CHA KWANZA 2023

Posted on: December 14th, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga inategemea kupokea jumla ya wanafunzi 2700 wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023. Hayo yamesemwa leo tarehe 14.12.2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mwanga Bi. Mwajuma A. Nasombe, alipokuwa akizungumza kwenye ziara ya kukagua madarasa mapya ya kidato cha kwanza, iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, Wilayani Mwanga. Amesema kwamba, Halmashauri ya Mwanga ilipokea kiasi cha Tsh. Milioni 180 kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa jumla ya madarasa mapya tisa. Madarasa hayo kwa sasa yamekamilika na tunachosubiri ni kupokea jumla ya wanafunzi 2700 wa kidato cha kwanza ili waweze kusoma, amesema Bi. Nasombe.

Akiwa katika ukaguzi wa madarasa hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, amesema kuwa, ameridhishwa sana kwa kazi nzuri illiyofanywa na viongozi wote wa Wilaya ya Mwanga, kwa kushirikiana na wananchi kwa kuhakikisha kwamba, ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati. “Madarasa yaliyojengwa ni mazuri sana, niwaombe tuyalinde vizuri na tuyatumie kwa ajili ya wanafunzi wetu, alisema Mkuu wa Mkoa’’. Akitoa pongezi kwa Serikali, Mhe. Babu alisema, anamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Mwanga fedha za ujenzi wa madarasa hayo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa ameendelea kusema, wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023 katika Mkoa wa Kilimanjaro, hakuna mwanafunzi hata mmoja atakayeshindwa kujiunga na masomo kutokana na ukosefu wa madarasa kwasababu, madarasa yaliyopo yanatosha kuwapokea wanafunzi wote watakaokuwa wamechaguliwa. Amewaagiza wazazi wote kuhakikisha kwamba, wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023, wanakwenda shuleni. Amisisitiza kwamba, kuanzia juma la pili baada ya shule kufunguliwa atatembelea shule na kukagua kama wanafunzi wamefika kwa ajili ya kuanza masomo.

Wilaya ya Mwanga ilipokea kiasi cha fedha Tsh. Milioni 180 mwanzoni mwa mwezi Octoba, 2022 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa. Shule zilizonufaika na fedha hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Kifaru madarasa mawili, Shule ya Sekondari Usangi Day madarasa mawili, Shule ya Sekondari Kwangu madarasa mawili, shule ya Sekondari Mgagao, madarasa mawili na shule ya Sekondari Vudoi Darasa moja. Madarasa hayo yameshakamilika yakiwa na viti pamoja na meza zake.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa