MHE. ANGELINA MABULA (MB) NAIBU WAZIRI WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ATEMBELEA WILAYA YA MWANGA NA KUKAGUA NAMNA MFUMO WA UKUSANYAJI WA MAPATO UNAVYOFANYA KAZI
Katika kuhakikisha kuwa Serikali ya awamu ya tano inafanya kazi kwa ufanisi mzuri kwa maendeleo ya wananchi wake, Mhe. Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametembelea Wilayani Mwanga na kuweza kukagua namna mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ardhi unavyofanya kazi. Mheshimiwa naibu Waziri kabla ya kufika Wilayani Mwanga aliweza kutembelea Wilaya ya Rombo eneo la Tarakea na kukagua eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliagiza kuwa Maafisa Ardhi wahakikishe wanafuatilia mapato ya ardhi kwa kila anayedaiwa na kuhakikisha kuwa wanawaandikia wadaiwa notisi kila baada ya miezi mitatu. Sambamba na hilo pia Naibu Waziri alisema, Maafisa Ardhi wahakikishe wanatoka mara tatu kwa wiki kwenda kutatua kero za ardhi kwa wananchi.
Hata hivyo Afisa Ardhi Msaidizi wa Wilaya Ndugu Salim Mhina amewashauri wamiliki wa ardhi ambao hawajalipia kodi wahakikishe wanafanya hivyo kabla sheria haijachukua mkondo wake.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa