TAARIFA YA OPRESHENI
Mwezi Septemba 29 – 20 octoba 2017, Wilaya ilitekeleza sheria ya kuithibiti Mifugo iliyoingizwa na kuikamata jumla ya Mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria ya kuthibiti magonjwa ya wanyama ya “Veterinary Act”. Kifungu cha 43 (a) na (b) ya mwaka 2003 na kutaifishwa na Serikali hadi kufikishwa katika mnada wa hadhara Mifugo 1,118 na iliyouzwa mnadani ni ng’ombe 1,113, punda mmoja (1) na Kondoo mmoja (1) na ng’ombe mmoja (1) alifia mnadani. Aidha, kupitia kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na ng’ombe wane (4) ilithibitishwa kuwa walikuwa wanamilikiwa na mfugaji mwenyeji ambaye alirudishiwa ng’ombe hao bila masharti yoyote.
Mnada uliendeshwa kwa kunadisha ngombe kwa mafungu ya ng’ombe ishirini ishirini kwa uwazi na ushindani. Bei ilitamkwa na mnunuzi aliyefikia bei ya juu aliuuziwa. Baada ya kuuza ng’ombe wote jumla ya TSH 238,080,000/= (milioni mia mbili thelathini na nane na elfu themanini) zilikusanywa ikijumuisha ushuru wa soko uliolipwa kwa Halmashauri ya Mwanga kwa kuuza ng’ombe 1,065 (elfu moja na sitini na tano) na kondoo 1 (mmoja). Ambapo punda mmoja hakuuzwa kwa kukosa mnununzi. Pesa zinajumuisha malipo yafuatayo:
Ushuru wa soko ulilipwa kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Own source akaunti namba 40210000551 iliyoko NMB Mwanga.
1.4 UPIGAJI CHAPA KWA MIFUGO (NG’OMBE)
Kwa kuzingatia agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu mnamo tarehe 15/06/2017 mkoani Dododma kwa maafisa Mifugo wote nchini linalohusu utambuzi na upigaji chapa wa mifugo ili kupanga matumizi bora ya ardhi na kumaliza migogoro ya watumiaji ardhi yakiwemo makundi ya wakulima na wafugaji.
Zoezi la upigaji chapa ng’ombe limeanza kutekelezwa tarehe 30/10/2017 katika Kata ya Kirya ambapo jumla ya ng’ombe 3,570 wamepigwa chapa.
Idadi ya ng’ombe waliopigwa chapa
KATA
|
KIJIJI
|
KITUO CHA UPIGAJI CHAPA
|
TAREHE
|
IDADI YA NG’OMBE SAJILIWA
|
Kirya
|
Kirya
|
Kirya
|
30/10/2017
|
216
|
01/11/2017
|
371
|
|||
02/11/2017
|
202
|
|||
Mangulai
|
04/11/2017
|
753
|
||
Mangulai
|
06/11/2017
|
929
|
||
Stafu
|
07/11/2017
|
482
|
||
Njiapanda
|
S/moyo
|
22/11/2017
|
617
|
|
JUMLA
|
3,570
|
1.5 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE
Changamoto
Baadhi ya viongozi hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa wataalam kuhakikisha wafugaji wote wanaleta mifugo yao kwa wakati muafaka ili kukamilisha zoezi la upigaji chapa mapema.
Mvua za vuli zilizoanza kunyesha zimekuwa zikikwamisha zoezi la upigaji chapa.
Wafugaji kuwapangia wataalam muda wa kufanya kazi kuwa ni kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 4:00 asubuhi kwa madai kuwa wanataka mifugo yao ikachunge.
Vyuma vya chapa kupinda.
Mifugo mingi kutokuwepo katika vijiji vyao mala baada ya kuhama kwenda kutafuta maji na malisho.
Namna ya kuzikabili
Sheria kali ikiwemo kutozwa faini isiyozidi milioni mbili (2,000,000/=) zitachukuliwa dhidi yao wote watakaokaidi zoezi hili nyeti na kuchelewesha kufanikisha zoezi la upigaji chapa wakati na baada ya zoezi kukamilika 30 Desemba 2017.
Halmashauri iliamuru kazi kufanyika kuanzia saa 12:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni kwa siku mbili tu na baada ya hapo wataalam kuhamia kituo kingine.
Halmashauri imechukua hatua za haraka kwa kuandaa vyuma imara na kazi kuendelea
Wafugaji wameshauriwa kurudisha mifugo yao kwakuwa mvua zimeanza kunyesha na majani kuchipua.
1.6 MIKAKATI
· Kutoa elimu kwa wafugaji wote wa Kata zote 20 za Wilaya ya Mwanga, ambapo mpaka sasa Kata za Kirya, Lang’ata, Kileo, Lembeni, Mgagao, Toloha, Mwanga, Kivisini, Jipe, Kigonigoni na Kwakoa kumeshafanyika mikutano ya kutoa elimu na uhamasishaji wa kupiga chapa.
·Kuzuia mifugo isiyo na chapa kuuzwa mnadani, kusafirishwa na kupelekwa machinjioni mala baada ya ratiba ya upigaji chapa mifugo kukamilika.
·Mala baada ya kumaliza kupiga chapa kwa kata na kijiji, timu ya wataalam inahamia Kata na vijiji vingine.
·Timu ya wataalam inapomaliza kupiga chapa eneo moja, Afisa mtendaji wa Kata husika kwa kushirikiana na mtaalam wa Mifugo wa Kata na viongozi wengine watafuatilia Mifugo yote ambayo haikupigwa chapa na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi kwa hatua zaidi za kisheria.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa