Kitengo hiki kina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa kazi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Halmashauri kwa vyombo vya habari. Majukumu mengine ni kufanya mawasiliano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, kuendeleza uhusiano baina ya Halmashauri na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Uhusiano wa Miji mingine.
Kitengo cha TEHAMA kinatoa huduma zake katika idara zote za Halmashauri pamoja na Taasisi zingine za serikali zilizopo ndani ya Halmashauri kama TASAF, Mamlaka ya Maji, Ukaguzi wa shule nk.
1. Kitengo cha Habari, na Mawasiliano kina jukumu la kuhakikisha
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya inadumisha
mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje.
2. Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli
za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya
ya Mwanga kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,
vitabu, vipeperushi, radio, TV na tovuti.
3. Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia,
kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.
Kusimika Mfumo wa Kompyuta wa Kuhifadhi taarifa na
Kumbukumbu za Watumishi na Mishahara (Intergrated
Human Capital Management System); pamoja na utekelezaji wa
Sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi
wa umma
4. Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kupokea na kushughulikia
malalamiko ya wadau yanayohusu Ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa