Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Elimu ya Watu Wazima kwa Mkoa wa Kilimanjaro yamefanyika mapema leo septemba 4, 2025 Wilayani Mwanga katika Shule ya sekondari St. Joseph.
Mgeni Rasmi wa hafla hii alikuwa Mhe. Rukia Zuberi, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Nurdin Babu.
Katika hotuba yake, Mgeni Rasmi alielezea umuhimu wa elimu ya watu wazima katika kupambana na ujinga, umaskini, na magonjwa ya kawaida ulimwenguni.
Pia kusisitiza kuwa shule zote za msingi na sekondari zinaweza kutumika kama vituo vya elimu ya watu wazima.
Kadhalika Mhe. Rukia Aliitumia fursa hii kuishukuru Halmashauri ya Mwanga kwa kuandaa maadhimisho haya ya kihistoria katika Mkoa wa Kilimanjaro. Vilevile, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na wote walioshiriki katika kuandaa maadhimisho haya.
Hafla hii ilikusanya viongozi mbalimbali, akiwemo afisa elimu wa Mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mwanga, wakuu wa idara za elimu ya msingi na sekondari, na maafisa elimu ya watu wazima kutoka Mkoa wa Kilimanjaro. Pia, walimu wa shule za msingi na sekondari, pamoja na wanafunzi wa elimu ya watu wazima kutoka vituo mbalimbali katika mkoa, walishiriki kikamilifu katika maadhimisho haya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa