Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mwanga Ndg. Robert Tarimo mapema leo Agosti 4, 2025 amefungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu na kufahamu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wote wa Uchaguzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku 3 kwanzia tarehe 4 hadi 6 Agosti 2025 katika ukumbi wa mikutano wa KKKT Mwanga Ndg. Robert Tarimo amewataka washiriki kusoma katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya katiba, sheria na maelekezo yanayotolewa na tume.
Kadhakika "Msiache kusoma katiba, sheria, kanuni, taratibu, miongozo na fuateni maelekezo mbalimbali yatakayotolewa na tume huru ya Uchaguzi ili kujiimarisha na kutekeleza kwa ufanisi majukumu yenu ambayo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewapa” ameongeza Msimamizi wa Uchaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa