Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha Desemba 2023 hadi Oktoba 2025, ikiwa ni matokeo ya usimamizi bora na utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa kuwaaga watumishi wa halmashauri, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bi. Zahara Msangi alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuiamini na kuiwezesha Halmashauri ya Mwanga kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika kipindi cha miaka miwili, mapato ya ndani ya halmashauri yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 3.07 mwaka 2023/2024 hadi Shilingi bilioni 3.97 kwa mwaka 2025/2026, sawa na ongezeko la zaidi ya shilingi bilioni 0.9 .

Ongezeko hilo limetokana na uimarishaji wa vyanzo vya mapato ikiwemo Mnada wa Mifugo Mgagao (kutoka Shilingi milioni 6 hadi milioni 13 kwa wiki), Masoko (kutoka Shilingi 250,000 hadi 1,200,000 kwa wiki), Machinjio(kutoka Shilingi 196,000 hadi 292,800 kwa wiki), na Vituo vya Afya (kutoka Shilingi 2,990,000 hadi 5,850,000 kwa wiki).

Katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Halmashauri imetekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 35, ikiwemo:
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya (Shilingi bilioni 3.8 ) na Jengo la Utawala*(Shilingi bilioni 3.6 ).

Shule mpya za Sekondari za Toloha (Shilingi milion 584.2 ) na Kilaweni (Shilingi milioni 584.3 ).
Mabweni ya wanafunzi katika shule za Kivisini, Ubangi, Kwangu, na Mgagao (jumla Shilingi milioni 814.3 ).

Kituo cha Afya Chomvu (Shilingi milioni 250 ) na Zahanati ya Toloha (Shilingi milioni 286.6 ).

Skimu za Umwagiliaji za Kirya (Shilingi bilioni 1.89 ), Kileo (Shilingi bilioni 4.8), na Kigonigoni (Shilingi bilioni 16.87 ).

Bi. Msangi alisisitiza kuwa mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri wa watumishi, madiwani, na wananchi wa Mwanga. Alimalizia kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuisaidia halmashauri hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa