Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, leo limepitisha rasimu ya bajeti ya Halmashauri yenye makisio ya Tsh. Bilioni 36.78. Baraza hilo la madiwani limepitisha bajeti hiyo huku wakikiri kwamba, ni bajeti ambayo imegusa maeneo yote ya msingi kuanzia ngazi ya jamii hadi uchumi wa mwananchi wa chini wa Wilaya ya Mwanga.
Akiwasilisha bajeti hiyo mbele ya Mkutano wa Baraza hilo la Madiwani, Mhe. Salehe R. Mkwizu, ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Diwani Kata ya Shighatini amesema kwamba, bajeti hii imebeba viapumbele mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutekeleza na kusimamia yaliyomo kwenye ilani ya chama tawala.
Mhe. Mkwizu pia amesema, pamoja na mambo mengine, bajeti hii imezingatia mambo mengi ikiwa ni pamoja na mpango wa maendeleo wa Taifa, mwongozo wa bajeti wa 2023/2024, kuboresha mazingira ya utendaji kazini, matumizi bora ya ardhi, upatikanaji bora wa huduma za afya, kuongeza uzalishaji wa mazao yenye tija, kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato na kuongeza ufaulu katika shule za msingi na sekondari.
Mambo mengine ambayo bajeti hii imezingatia ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi, kuboresha miundombinu ya mifugo na uvuvi, kudhibiti mapato ikiwa na pamoja na kuongeza kasi katika kukusanya mapato ya Serikali, kuboresha miundombinu pamoja kukuza fursa za ajira.
Aidha, katika hotuba yake ameendelea kusema kwamba, Halmashauri ya Mwanga, kwenye makusanyo ya mapato ya ndani imekadiria kukusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 2.9 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyoko ndani ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa