Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga leo tarehe 03 Agosti, 2021 itaanza kutoa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO kwa wananchi wake.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Dr. Abdul M. Msuya, yeye pamoja na watumishi wake wa Idara ya Afya wapejipanga vyema kuhakikisha kuwa huduma inatolewa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na hakuna atakaye acha kupatiwa huduma kama ana sifa za kupata.
Mganga Mkuu amesema kwamba, chanjo itatolewa katika vituo vya Afya vya Mwanga, Kigonigoni na Hospitali ya Wilaya ya Usangi. Sambamba na zoezi hilo, watakaohusika kupatiwa chanjo ni watumishi wa afya, watu wenye magonjwa sugu na wazee wenye umri wa miaka 50 na kuendelea.
Aidha amesema, ili mtu aweze kupatiwa huduma ya chanjo ni lazima awe amejisajili kwenye mfumo maalum ili aweze kupata namba ya utambulisho, ambapo mfumo huo ni https://chanjocovid.moh.go.tz. Wakati wa kujisajili mteja anapaswa kuwa na vitambulisho moja wapo kati ya kitambulisho cha Taifa, kura ama leseni ya udereva.
Pamoja na hayo, kabla mteja hajapata chanjo, atapaswa kujaza fomu maalum ya hiari ya kuchanjwa na mara baada ya kuchanjwa atapaswa kurudi kwenye kituo alichopata huduma siku ya tatu, ya saba na ya ishirini na moja ili wataalamu waendelee kuangalia mwenendo wa afya ya mchanjwaji. Baada ya chanjo, mteja atapatiwa kadi maalum ya chanjo kadi ambayo ni kieleezo chake kuwa amesha chanjwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa