Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Mwanahamisi Munkunda ameongoza Kongamano la mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayofanya kazi ndani ya Wilaya ya Mwanga kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za mashirika kwanzia mwaka 2021 hadi 2025 kwa kuangazia mafaniakio, changamoto, fursa na matarajio ya kila shirika.
Katika Mkutano huo uliofanyika leo tarehe 18 Juni 2025, katika Ukumbi wa TRC, DC Munkunda amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kazi kubwa na mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuwa ni wadau muhimu katika kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Kadhalika Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Zahara Msangi amewataka wadau hao wa maendeleo Kuimarisha ushirikiano na Serikali ili kuleta tija katika utekelezaji wa Miradi yao na hivyo kuleta mafanikio tarajiwa katika jamii
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa