Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Mwanga imetoa mkopo kiasi cha Tsh. 15,000,000 kwa vikundi sita vya ujasiriamali vilivyopo ndani ya Wilaya ya Mwanga. Vikundi vilivyofaidika na mkopo huo vinatoka Kata za Kivisini, Kigonigoni na Ngujini.
Akisoma taarifa ya kiasi kilichotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake na Vijana kwa mwaka wa fedha 2017/18 Bi. Wahilina Salum Afisa Maendeleo ya Jamii alisema, Halmashauri imetenga kiasi cha Tsh. 122,822,526.00 kutoka katika mapato yake ya ndani na hadi sasa kiasi cha Tsh. 40,190,390.07 kimeshatolewa kwa mifuko hiyo. “ Leo hii tunategemea kutoa mkopo wa Tsh. 15,000,000 kwa vikundi sita vya akina mama na tarehe 08 Machi,2018 ambayo itakuwa siku ya wanawake Halmashauri inatarajia kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000 alisema Bi. Wahilina Salum.
Akizungumza na wanufaika wa mkopo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Ndg. Golden A. mgonzo amewapongeza akina Mama waliopatiwa mkopo huo na kutoa wito kwa wanawake wa Wilaya ya Mwanga kuomba kukopeshwa kwani ofisi yake ina fedha za kutosha.
Kabla ya zoezi la kugawa mkopo huo kuanza Mwanasheria wa Halmashauri Ndg. Mhendeli Wilson Msaki alisisitiza kwa wanufaika kuwa mkopo unaotolewa kwao siyo msaada bali ni fedha ya Serikali na inapaswa kurejeshwa kwa mujibu wa mkataba. Mwanasheria aliendelea kusisitiza kuwa kila kikundi kilichonufaika na mkopo kitawajibika katika kurejesha na kila mtu mmoja mmoja kwenye kikundi atawajibika.
Nao wanufaika wa mkopo huo wametoa shukrani kwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kuhakikisha kuwa inawanyanyua akina mama kimaisha na hii inawajengea mtazamo chanya kwa Serikali kwamba inawajali na kuwathamini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa