Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kupitia Idara ya Elimu Msingi na Sekondari wanatarajia kuwa na juma la elimu tarehe 11 Julai, 2018. Juma hilo ambalo litahusisha wadau mbalimbali wa Elimu litafanyika katika Kata ya Lembeni.
Akizungumza ofisini kwake Kaimu Afisa Elimu Msingi, Bi. Prisca Mushi amesema, juma hili la elimu litahudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanafunzi, walimu, waratibu elimu kata, wazazi wa wanafunzi pamoja na waalikwa wengine ambao watawakilisha wadau wa elimu.
Ameendelea kusema, lengo kubwa la juma hili ni kuhamasisha jamii kushiriki katika kuboresha utoaji wa elimu bora, kupongeza jitihada za shule na wanafunzi wanaofanya vizuri na kujadili changamoto na mafanikio ya kielimu kwa jamii ili kuunga mkono jitihada za Serikali.
Katika maadhimisho hayo kutakuwepo na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwasilishwaji wa taarifa ya elimu katika Wilaya, maenesho ya shughuli za kielimu, michezo na burudani yenye lengo la kuboresha na kuinua ari ya jamii kushiriki katika maendeleo ya elimu, utoaji wa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri katika utekelezaji wa KKK na matokeo mazuri ya mtihani wa darasa la VII MOCK, kidato cha nne na kidato cha sita.
Hata hivyo Kaimu Afisa Elimu amewaomba na kuwasisitiza wadau wa elimu watakao alikwa wahakikishe wanahudhuria watakapo pata mualiko wa kushiriki kutoka ofisi ya Mkurugenzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa