Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, ni miongoni mwa halmashauri za Mikoa ya Tanzania Bara zinazotegea kufanya mtihani wa kidato cha nne utakao anza kufanyika tarehe 05 Novemba, 2018 na kumalizika tarehe 23 Novemba, 2018.
Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya Mwanga, Ndg. Chacha Megewa amesema kuwa, kutakuwa na jumla ya vituo vya kufanyia mitihani 44, na jumla ya watahiniwa 3266 wa sekondari (School Candidates), wanategemea kufanya mtihani wa kidato cha nne ambapo, wavulana ni 1471 na waschana wakiwa ni 1795.
Afisa Elimu ameendelea kusema, pia patakuwepo na watahiniwa wa kujitegemea 270 ambao watafanya mtihani kama wanafunzi wa kujitegemea (Private Candidates/PC), wavulana wakiwa ni 118 na wasichana 152. Pia watakuwepo jumla ya wanafunzi 21 watakao fanya mtihani wa maarifa (Qualifying Test/QT), wavulana wakiwa ni 8 na wasichana ni 13.
Kwa ujumla wake Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga inategemea kuwa na watahiniwa wa mtihani wa sekondari, kujitegemea na watahiniwa wa mtihani wa maarifa. Ndg. Megewa amesema kuwa, jumla ya watahiniwa wote watakuwa 3557 ambapo, wavulana watakuwa 1597 na wasichana watakuwa 1960.
Kuhusu maandalizi ya mtihani huo, Afisa Elimu amesema, maandalizi yote kwa sasa yako vizuri na wanasubiri tarehe ya kufanya mtihani ili zoezi liendelee. Hata hivyo, amewatakia kila la heri watahiniwa wote wanaotegea kufanya mitihani yao na kuwasisitiza kufanya mitihani katika hali ya utulivu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa