Kamati ya Elimu Afya na Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga leo imepitia na kukagua miradi ya elimu na afya inayo endelea kujengwa Wilayani Mwanga. Kamati hiyo, imepitia jumla ya miradi minne. Miradi iliyopitiwa na kukaguliwa ni ujenzi wa bwalo na ukarabati wa bweni katika shule ya sekondari Nyerere, umaliziaji na ukarabati wa kituo cha afya Kisangara na ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya.
Akizungumza kwa niaba ya wanakamati wenzake, Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Lembeni, Mhe. Alex Mwaipopo amesema kwamba, wanampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Mwajuma A. Nasombe, pamoja na timu yake ya wataalamu kwa kazi kubwa na nzuri, wanayo ifanya, katika kusimamia miradi ya Halmashauri vizuri. Ameendelea kusema kwamba, miradi ni mizuri na inaonekana kabisa kwamba, usimamizi wake upo sawa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Shighatini Mhe Dr. Salehe R. Mkwizu, amesema kwamba, miradi mingi ya Halmashauri ipo vizuri kwa kila hatua. “Naomba niseme kwamba miradi tuliyo tembelea leo, ni mizuri, inaridhisha na thamani ya fedha inaonekana, alisema Dr. Mwizu”.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa