Katika kuhakikisha kwamba jamii inapata lishe iliyo bora, hasusani watoto wadogo, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga leo imezindua rasmi Kamati ya Lishe ya Wilaya itakayokuwa inahusika na usimamizi wa lishe hapa Wilayani.
Kamati ya Lishe Wilaya, imeundwa na wajumbe wafuatao; Mkurugenzi Mtendaji, Mganga Mkuu Wilaya, Afisa Lishe, Afisa Utumishi, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari. Wajumbe wengine ni Mwasibu Mkuu, Afisa Mipango, Afisa Kilimo, Afisa Uvuvi na Mifugo, Mwandisi wa Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii na NGO's, CBO's na FBO's. Wajumbe wa kamati hii, kila mmoja anawajibika kwa kuhakikisha kuwa lishe bora inapatikana sambamba na kutoa taarifa mbalimbali zitakazosaidia upatikanaji bora wa lishe.
Akieleza sababu za utapiamlo, Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Christina L. Guveti alieleza kuwa, watoto wengi wanapata tatizo la utapiamlo kutokana na lishe duni, uhaba wa chakula, uangalifu hafifu wa watoto toka kwa wazazi wao pamoja na ukosefu wa huduma bora za afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa