Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi Dr. Rashid Tamatama ashiriki kuteketeza nyavu haramu zinazotumika kuvulia Samaki katika Bwawa la Nyumba ya Mungu. Katika uteketezaji wa Nyavu haramu, katibu mkuu alipokea taarifa inayonesha katika operesheni jumla Tsh. 203 milioni ilikusanywa kama tozo za faini kwa watuhumiwa zilikushunywa na kupelekwa serikali kuu, huku magari 8 na pikipiki 2 zinashikiliwa katika kituo cha Polisi Mwanga, magari na pikipiki ni zilizokuwa zikijihusisha kwenye Uvuvi Haramu.Pia katika taarifa hiyo ilionesha Mapato ya Halmashauri kuongezeka, kwani Uvuvi haramu umepungua na zana za uvuvi kusajiliwa. Katibu Mkuu aliagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu viongozi na wataalamu wanaojihusisha na uvuvi haramu.Mwisho aliahidi kufuatilia namna ya kuwawezeha wananchi wa eneo husika namna ya kufanya shughuli mbadala pale Bwawa linapofungwa au samaki wanapopungua.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa