Mbunge na Waziri wa Mali asili na Utalii Prof. J.A. Maghembe aja mpango wa kuondoa uhaba wa Waalimu wa sayansi na Kiingereza katika Jimbo lake la Mwanga kwa kuandaa mpango wa kuutumia Mfumo wa TEHAMA utakaomwezesha Mwalimu mmoja kufundisha shule zaidi ya kumi kwa wakati mmoja. Hayo aliyasema tarehe 2/09/2017 alipowaalika Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri, Wakuu wa Shule pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga. Alisema atatumia zaidi fedha za Mfuko wa Jimbo pamoja fedha za Marafiki zake ambapo amewaombo wamsadie ili kuongeza ufaulu na Uelewa wa masomo kwa Wanafunzi wa shule za sekondari.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa