• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

KIWANDA CHA KILIMANJARO BIOCHEM CHAPEWA MWAKA MMOJA NA MHE. NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE

Posted on: March 10th, 2018

Naibi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (MB) jana alifanya ziara yake Wilayani Mwanga na kuweza kutembelea kiwanda cha Kilimanjaro Biochem kinachojihusisha na uzalishaji wa spiriti na baadae kutembelea Ziwa Jipe ambalo linatumiwa na nchi ya Tanzania na Kenye.

Katika ziara yake hiyo ambayo aliambatana na maafisa mbalimbali wa Serikali wakiwemo Maafisa wa mazingira aliweza kukitembelea kiwanda cha Kilimanjaro Biochem na kujionea namna kiwanda hicho kinavyoendesha shughuli zake za uzalishaji. Sambamba na kujionea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi aliweza kukagua mazingira ya kiwanda na kutaka kujua kama wamiliki wa kiwanda wanafuata sheria za utunzaji wa mazingira kama sheria namba 20 ya mwaka 2004 inavyotaka.

Katika ukaguzi wake Mhe. Naibu Waziri aligundua kuwa maji taka ya kiwanda bado yana virutubisho vingi ambavyo ni hatari kwa mazingira na viumbe vyake kwa ujumla. Mhe. Naibu Waziri aliendelea kusema Serikali haita kaa kimya kama kiwanda hicho hakitaweka utaratibu na mfumo wa kutibu maji machafu na aliagiza mfumo wa kutibu maji hayo uwekwe ndani ya mwaka mmoja. “Natoa agizo kuwa mfumo wa kutibu maji machafu uwekwe na ukamilike ndani ya mwaka mmoja la sivyo kiwanda tutakifunga kama mtashindwa kutekeleza” alisema Naibu Waziri. Hata hivyo alisema maji machafu yanayotoka kiwandani hapo yana uwezo wa kuzalisha mbolea hivyo wamiliki wa kiwanda wafanye utafiti kwa kushirikiana na wataalamu kutoka chuo cha SUA ili waone ni namna gani mbolea hiyo inaweza kuzalishwa na kuweza kuwanufaisha watanzania.

Pamoja na dosari aliyoiona kiwandani hapo Mhe. Naibu Waziri hakuacha kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa kiwanda Ndg. Joshipura A.P kwa kuweza kutoa ajira zaidi ya 100 kwa wazawa na kuchangia miradi ya maendeleo kwa jamii inayozunguka kiwanda. Pia alitoa pongezi na shukrani kwa juhudi zilizochukuliwa na uongozi wa kiwanda kwa kuhakikisha kuwa hakuna hewa ya ukaa inayotoka kiwandani kitu ambacho ni kizuri katika utunzaji wa mazingira.

Akitoa shukrani zake kwa Serikali Mkurugenzi wa kiwanda cha Kilimanjaro Biochem Ndg. Joshipura A. P alisema “tumeyapokea maelekezo tuliyopewa na Mhe. Naibu Waziri na tunaahidi kwamba ndani ya mwaka mmoja tutayafanyia kazi kwani mwaka mmoja tuliopewa unatutosha”, alisema Ndg. Joshipura.

Akiwa ziwa Jipe Mhe. Naibu Waziri alijionea namna magugu maji yalivyosambaa katika ziwa hilo ikiwa sehemu kubwa ya magugu maji yapo upande wa Tanzania kuliko upande wa Kenya. Mhe. Naibu Waziri alisema kwa sasa kuna haja kubwa kwa Serikali kuhakikisha wanashughulika na magugu maji yaliyopo ziwa Jipe. Mhe. Naibu Waziri alisema mwaka 2017 Machi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba alitembelea Ziwa hilo na kujionea hali ilivyo hivyo anaamini ujio wao wote utakuwa siyo wa bure.

Mhe. Naibu Waziri alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya milimani ili wawe na kilimo cha uhifadhi ambapo wataepusha mmomonyoko wa udongo ambao unachangia ziwa kupungua kina. Pia alisema Mkurugenzi ahakikishe panakuwepo na kamati za mazingira kuanzia ngazi ya Kitongoji ili ziweze kusimamia na kuhakikisha hakuna uharibifu wa mazingira. Sambamba na hilo alisema Serikali kwa sasa inafanya operesheni kubwa juu ya uvuvi haramu hivyo wavuvi wajihadhari na uvuvi huo na wahakikishe wanakuwa na leseni za uvuvi.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa