Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mhe. Tadayo Anania amemuagiza Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mwanga kuhakikisha kuwa anatenga Hekari 54 kwa ajili ya kujenga Hospitali mpya ya Wilaya ya Mwanga, kutenga hekari 25 kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana ya Mkoa, kutenga ardhi kwa ajili ya kujenga mahakama mpya ya Wilaya na kutenga ardhi kwa ajili ya kujenga stendi ya mabasi.
Mhe Tadayo ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza la Halmashauri uliokaa leo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanga.
Hata hivyo Kaimu Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mwanga Ndg Salim H. Mhina amesema kuwa, maelekezo aliyopatiwa na Mhe Mbunge atayafanyia kazi. Amesema kuwa eneo la kujenga hospitali ya Wilaya lipo tayari na eneo la kujenga shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa nalo lipo tayari. Emeendelea kusema kuwa ardhi kwa ajili ya kujenga stendi nalo lipo tayari. Kuhusu eneo la kujenga mahakama ya Wilaya, ndg Mhina alisema, eneo lipo lenye ukubwa wa hecta 1.254 kiwanja namba 161 kitalu 'A'.
Aidha, kuhusu suala upatikanaji wa umeme katika vijiji vya Mwai na Karambandea Mhe. Mbunge amesema kuwa suala hili lipo katika hatua nzuri. Amesema, Waziri mwenye dhamana ameahidi kufika katika vijiji husika na kuhakikisha vinapatiwa umeme.
Pia ameendelea kusema kuwa, katika sekta ya Kilimo, mradi wa umwagiliaji wa Kambi ya Swala uliopo katika kata ya Kirya, serikali imeupatia kiasi cha shilingi milioni mia nane.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa