Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mhe. Joseph Tadayo Anania, ametoa pongezi kwa viongozi watendaji na viongozi wanasiasa, wa Wilaya ya Mwanga, kwa kujitoa kwa moyo, katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo, ambayo imekuwa ikitekelezwa ndani ya Wilaya ya Mwanga.
Mhe. Mbunge ametoa pongezi hizo leo tarehe 20.09.2023 kwa nyakati tofauti na maeneo mbalimbali alipokuwa katika kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo la Mwanga.
Akitoa pongezi zake kwa viongozi hao, Mhe. Mbunge amesema, Wilaya ya Mwanga ina viongozi sahihi, ambao ni wachapakazi, wanaojituma na wenye uzalendo wa kuwatumikia wananchi wa Mwanga muda wote. Ameendelea kusema kwamba, serikali ya awamu ya sita imeleta miradi mingi hapa Mwanga na miradi mingine itaendelea kuja, nitoe wito kwa viongozi kuendelea kuisimia miradi hii vizuri na itunzwe vizuri pia, amesema Mhe. Mbunge.
Mhe. Mbunge atakuwa na ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ambapo leo, ameanza ziara ya kutembelea na kukagua jumla ya miradi saba ambayo ni Jengo la Utawala la Halmashauri, Shule za Msingi Mwai, Rangaa, Kifula, Kivindu na shule za sekondari Msangeni na Kigonigoni.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa