Shule ya wasichana ya Dr. Asharose Migiro ni miongoni mwa shule zinazovutia kwa namna miundombinu ya shule hiyo inavyo zidi kujengwa mithili ya uyoga unaoota na kukuwa ndani ya muda mfupi. Ni ndani ya muda wa miaka miwili tu shule hii tayari imesha kamilisha majengo mawili ya maabara na jengo la utawala.
Mwezi Novemba 2017, shule hiyo ilipatiwa na wafadhili kiasi cha shilingi 124,368,104/=, (milioni miamoja na ishirini na nne laki tatu sitini na nane na mia moja na nne), fedha ambazo zimetumika kujenga jengo la utawala. Jengo hilo lilianza kujengwa mwezi novemba 2017, na kukamilika mwezi Aprili 2018 na sasa jengo hilo linatumika. Hadi kukamilika kwa jengo hilo, limetumia kiasi cha shilingi milioni mia moja ishirini na tatu, mia nane na nane elfu na mia sita hamsini (123,808,650/=). Jengo hili la utawala limejumuisha ofisi ya Mkuu wa Shule, Makamu Mkuu wa Shule, Ofisi za Idara za Taaluma pamoja na sehemu ndogo ya kukutana walimu.
Pamoja na muonekano mzuri wa mandhari ya shule hiyo, pongezi nyingi zinapaswa kumuendea Mkuu wa Shule hiyo, kwa namna anavyo simamia vizuri miradi ya maendeleo ya shule inayoletwa na wafadhili shuleni hapo kwani, amekuwa mfano mzuri wa kuigwa hata na viongozi wengine pamoja na jamii kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa