Mkoa wa Kilimanjaro ni moja wapo kati ya Mikoa iliyoshoriki katika Tamasha la Utamaduni la Kitaifa lililo andaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, tamasha ambalo limefanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 01 Julai na kuhitimishwa leo tarehe 03 Julai, 2022.
Tamasha hilo ambalo lilipambwa na ngoma za Utamaduni, Vyakula vya asili na zana mbalimbali za kale, lilifunguliwa rasmi tarehe 02 Julai, 2022 na Waziri Mkuu wa Tanzania (Mb) Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kufungwa rasmi leo tarehe 02 Julai, 2022 na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mhe. Mohamed O. Mchengerwa.
Katika tamasha hilo, Mkoa wa Kilimanjaro umeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika maandalizi ya vyakula vya asili na kuweza kupewa zawadi ya cheti, ngao na kiasi cha fedha Tsh. milioni moja na laki mbili.
Mkoa wa Kilimanjaro umewakilishwa na kikundi cha sanaa na utamaduni kutoka Wilaya ya Mwanga kijulikanacho kwa jina la "Kikundi Teule". Kikundi hiki kiliteuliwa na mkoa kutokana na kazi zake nzuri za uhifadhi wa utamaduni ambazo kimekuwa kikifanya mara kwa mara haswa katika jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa