Mkuu wa wilaya ya Mwanga Mhe. Rukia Zuberi amezindua rasimi zoezi la uandikishaji na ugawaji wa bima ya Afya kwa wote kwa awamu ya kwanza.
Zoezi hilo la uzinduzi limefanyika tarehe 14 Februari 2026 katika ofisi ya mamlaka ya mji mdogo huku likiendelea katika kata zote za wilaya ya Mwanga, likilenga zaidi watu wenye uhitaji maalumu kwa awamu ya kwanza, huku takribani kaya 1709 zimekusudiwa kunufaika na huduma ya bima ya Afya kwa wote kwa awamu ya kwanza.
Aidha, mkuu wa wilaya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri na kutenga bajeti kwa ajili ya bima ya afya kwa wote kwa wilaya ya Mwanga, huku akiwataka wananchi kuunga jitihada za raisi kwa kujiandikisha ili waweze kupata huduma ya bima ya afya kwa wote.
Aidha, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mwanga Bi Mwashabani Mrope kwa maandalizi mazuri ya zoezi la uzinduzi wa bima ya afya kwa wote, huku akisisitiza wahudumu wa afya katika kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Naye diwani wa kata ya Mwanga Mhe. Hinja Solomon Msuya ameishukuru Serikali kwa kuipa heshima kata ya Mwanga kwa kuichagua kuwa moja ya eneo la uzinduzi wa bima ya afya kwa wote kwa wilaya ya Mwanga.
Aidha,Mganga mkuu wa wilaya ya Mwanga Selijo Kusekwa amesema wananchi wenye bima watakuwa na uwezo wa kupata huduma ya matibabu kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, Hospitali ya wilaya na rufaa kwa kufuata utaratibu maalumu wa rufaa.
Sambamba na hayo wananchi wameishukuru sana serikali kwa kujali uwepo, ustawi na afya zao kwa kuwaletea huduma ya bima ya afya kwa wote.













Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa