Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Ndg. Golden A. Mgonzo, jana alikabidhi ofisi rasmi kwa Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Ndg. Zephrin Lubuva. Makabidhiano hayo ambayo yalifanyikia kwenye ukumbi wa TRC-Mwanga, yaliweza kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Aaron Y. Mbogho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga, Mhe. Theresia P. Msuya na Wakuu wa Idara zote za Halmashauri.
Akiwa anakabidhi Ofisi Ndg. Mgonzo alitoa shukrani za dhati kwa watumishi wote kwa namna walivyompa ushirikiano kipindi chake chote cha uongozi hapa wilayani Mwanga. Aliwaomba wakuu wa idara waendelee kumpa ushirikiano Mkurugenzi mpya ili kazi zake ziweze kwenda vizuri.
Aidha Ndg, Mgonzo hakuacha kumshauri Mkurugenzi aliyechukua nafasi yake kuhakikisha kuwa, anasimamia vizuri mapato ya Halmashauri. Alisema kuwa Halmashauri ina vyanzo vingi vya mapato hivyo ni vyema vikasimamiwa vizuri. Alisema kuwa, Halmashauri iendelee kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuendelea kuongeza mapato ya ndani.
Ndg. Mgonzo alikabidhi ofisi jana ikiwa ni sehemu ya taratibu za utumishi wa umma, kwa pale mtumishi anapo ondoka kwenye ofisi kuhakikisha kuwa anakabidhi kwa mamlaka husika.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa