Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Mwanga Bwana Golden. A. Mgonzo aliitisha mkutano wa kiutendaji kazi kwa watendaji wa kata na vijiji ili watoe changamoto wanazokutana nazo kazini. Katika kikao hicho alikuwepo Mkuu wa Wilaya Mhe. A.Y. Mmbogho pamoja na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo vya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ambapo ilifanyika tarehe 11/01/2018 katika ukumbi wa waalimu (TRC Mwanga). Katika kikao hicho watendaji wapya wa vijiji waliwasilisha changamoto mbalimbali ,hata hivyo afisa Mtendaji wa kijiji cha ngulu aliwajibishwa kwa kulipishwa faini kwa kukosa makosa mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira katika kijiji chake.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji aliwataka kufuata kanuni, sheria na taratibu za kazi zao,pia wawe wanawafuatilia watumishi wa umma waliopo maeneo yao ya kazi kwani wao ndio wanaomwakilisha katika vijiji na kata husika. Pia aliwataka wawe wanawasilisha taarifa ya kila mwezi ya utendaji kazi pamoja na taarifa ya vikao vya kisheria, taarifa ya mapato na matumizi ya kila mwezi. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. A. Y. Mmbogho aliwashauri kuwa wanajisomea mambo mbalimbali ili kupata uelewa wa kawaida ili kuepuka kupokea taarifa isiyo sahihi kwa kutokujua.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa