Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilayani Mwanga na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa na ametoa pongezi kwa Viongozi wa Wilaya ya Mwanga kwa kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za serikali.
Mhe. Babu amezungumza hayo leo Juni 13, 2025, wakati wa ziara ya kukagua miradi itakayopitiwa na mbio za Mwenge Uhuru kwa mwaka huu, na kusisitiza kuwa Mkoa wa Kilimanjaro upo mstari wa mbele katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.
Aidha, Mhe. Babu ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kupeleka miradi mingi ya maendeleo katika mkoa wa Kilimanjaro, jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za kijamii kwa Wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa