Leo Wilaya ya Mwanga imeadhimisha siku ya Mashujaa kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa mbalimbali ambao walihusika katika kuipigania nchi na Taifa la Tanzania. Maadhimisho hayo yaliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdallah Mwaipaya kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
Maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la kufanya usafi katika eneo la ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Mwanga kwa kuwahusisha watumishi wa Serikali, Wananchi, Viongozi wa Dini, Viongozi wa mila na wazee.
Katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya alihutubia kwa kusema kwamba “Leo ni siku muhimu sana kwa Taifa letu, kwani tunawakumbuka Mashujaa wetu ambao walipambania Taifa letu la Tanzania.” Aliendelea kusema kwamba, mashujaa hawa walipoteza uhai kwa ajili ya uzalendo wa kweli waliokuwa nao.
Mhe. Mkuu wa Wilaya aliendelea kusema kwamba, mashujaa hao walipambana kwa dhati dhidi ya wadhalimu wa nchi na ndiyo maana Taifa letu lina Amani ambayo ilitokana na ushujaa wao. Amewaomba Watanzania kuendelea kuwaombea mashujaa hao ambao kwasasa walisha tangulia mbele ya haki. Pia amewataka watanzania kutafakari juu ya umuhimu wa mambo mazuri waliyo yapigania mashujaa hao, kuyaiga na kuyarithisha kwa vizazi vijavyo ili wafurahie tunu ya Amani tuliyo nayo
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa