Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mnada wa mifugo wa Mgagao uliopo Wilayani Mwanga, ulikosa wafanyabiashara wa mifugo kwa wiki mbili mfululizo na kupelekea Halmashauri kuingia hasara kwa kupoteza mapato.
Sababu iliyopelekea mnada huo kukosa wafanya biashara, ni baada ya kuibuka kwa mgogoro kati ya wafugaji wa jamii ya kimasai na wakulima na kupelekea wafugaji kususa kuleta mifigo yao katika mnada huo.
Hata hivyo, Serikali imeweza kuutatua mgogoro huo kwa kushirikiana na jamii ya wafugaji na wakulima. Katibu wa jamii ya wafugaji Wilayani Mwanga Ndg. Peter Martini Moleli amesema kuwa, kuanzia ijumaa ya tarehe 06.09.2019, watarejea rasmi kwenye mnada wa mgagao na wataleta mifugo ya kutosha. Katibu huyo ameendelea kusema kuwa, wataendelea kuheshimu wafugaji na kuheshimu sheria zilizowekwa na Serikali kwa manufaa na maendeleo ya wilaya yao ya Mwanga.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Ndg. Zefrin K. Lubuva, amewaahidi wafugaji na wafanya biashara ya mifugo kuwa, kwasasa atahakikisha kuwa anaboresha mnada huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo wafanya biashara wa mifugo. Pia amesema, ataendelea kusimamia kikamilifu mapato yanayotokana na mnada huo na kurudisha asilimia ya mapato hayo kwenye jamii ya wafugaji na wakulima, ili kuendeleza miradi ya kijamii inayozunguka jamii hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa