Hatimaye ile siku adhimu ya kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika leo imekamilika baada ya viongozi na wananchi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Mwanga kushiriki siku hiyo katika kituo cha malezi ya watoto COMPASSION kilichopo Kijiji cha Lang'ata Bora.
Katika kuadhimisha siku hii, watoto walipata fursa ya kuonesha vipaji mbalimbali kwa kucheza, kuimba na kuruka sarakasi.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mhe. Mwanahamisi Munkunda, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema kila Mzazi au Mlezi ana wajibu wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kusimamia na kuhakikisha watoto wanapata haki zao zikiwemo malezi na elimu kwani tayari Mh, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha, kuboresha na kuongeza miundombinu rafiki.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mwanga Bi Zahara Msangi amewakumbusha Wazazi kutenga muda kwa ajili ya kuzungumza na watoto wao. Alisema ni vema Wazazi wakajenga urafiki na watoto wao ili wawe huru kuwaeleza changamoto wanazokabiliana nazo hususan ukatili na unyanyasaji wanaokutana nao.
Maadhimisho hayo Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo, "Haki za Mtoto Tulipotoka, tulipo na tuendako"
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa