Kituo cha afya cha Kisangara kilichopo Kata ya Lembeni, kimenufaika kwa kupata Milioni 400 kutoka serikalini. Fedha hizo zimetumika kujenga majengo mapya manne ambayo ni maabara, upasuaji, wazazi (maternity) na mochwari. Katika kuhakikisha ujenzi na usimamizi wa miundombinu hiyo unakwenda vizuri, ziliundwa kamati maalumu ambazo ni kamati ya manunuzi, ujenzi na mapokezi.
Akielezea hatua za ujenzi zilipofikia hadi mwishoni mwa mwezi juni, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Ndugu. Orest Peter alisema, mpaka sasa majengo hayo yapo kwenye hatua ya kufanyiwa "finishing".
Aidha Ofisi ya Mkurugenzi imedhamiria kuongeza kiasi cha shilingi milioni 21 ili kuhakikisha kuwa umaliziaji wa majengo hayo unakuwa katika hali nzuri na ya kupendaza. Mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 10 kimesha changiwa na ofisi ya Mkurugenzi kwenye kituo hicho cha afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa