Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imepatiwa kiasi cha Tsh. 230,000,000/= (milioni miambili na thelathini) na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Vudoi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga Bi. Mariana Sumari, ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Kamati ya Fedha kilicho kaa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mapato na matumizi ya Halmashauri.
Fedha hizi zimefika, ikiwa ni wiki moja tu imepita, toka Waziri wa TAMISEMI, Mh. Sulemani Jafo kutoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa, fedha zilizo tumwa kwenye Halmashauri mbalimbali na TAMISEMI, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni ya kidato cha tano, wahakikishe zinasimamiwa vizuri na ujenzi wake ukamilike kwa wakati ulio wekwa.
Kiasi hiki cha fedha, kitatumika kujenga vyumba vinne vya madarasa ambavyo vitakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 160 pamoja na ujenzi wa mabweni mawili ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 40 kwa kila bweni.
Katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa mabweni na vyumba hivyo vya madarasa unakamilika kwa wakati, Halmashauri tayari imesha tangaza tenda ya ujenzi wa miundo mbinu hiyo ili ifikapo tarehe 30 Agosti, 2018, ujenzi uwe umesha kamilika na kuweza kuwapatia fursa wanafunzi wa kidato cha tano kupata nafasi ya kuendelea na masomo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa