• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mwanga District Council
Mwanga District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na rasilimali watu
      • Afya
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii na Uhusiano
      • Ujenzi na zima moto
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali asili
      • Mazingira
      • Mamlaka ya Mji mdogo
    • Vitengo
      • Teknolojia Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Fursa za Kilimo
    • Fursa za Uvuvi
    • Fursa ya Madini
    • Fursa ya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za kisheria
    • Huduma za kuwawezesha wajasiria mali
  • Madiwani
    • Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mipango mikakati
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Halmashauri
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

SIKU NANE TU, OPERESHENI YA KUKABILIANA NA UVUVI HARAMU BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU YAIINGIZIA SERIKALI MILIONI 95,720,000/=

Posted on: October 27th, 2018

Operesheni ya kukabiliana na uvuvi haramu, inayofanywa na wizara ya Mifugo na Uvuvi katika bwawa la Nyumba ya Mungu, lililoko Wilayani Mwanga, imeweza kuiingizia serikali kiasi cha Tsh. 95,720,000. Hayo yamesemwa na Kamanda wa operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu Ndg. Ranwel Mbukwah.

Akisoma taarifa ya operesheni hiyo, mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Hamisi Ulega, kamanda huyo alisema, kiasi hiki cha mapato ambacho ni kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi kimetokana na faini mbalimbali walizotozwa, wavuvi ambao wamekamatwa wakiwa wanajihusisha na uvuvi haramu. Operesheni hii ambayo ilianza tarehe  18 Octoba, 2018 imekuwa ya manufaa sana, kwani jumla ya watuhumiwa 84 wamekamatwa na kati ya hao, watuhumiwa 83 wamelipa faini na mtuhumiwa  mmoja ameshindwa kulipa faini na yupo kwenye vyombo vya sheria, pikipiki zinazofanya biashara haramu zimekamatwa, na samaki wachanga wameweza kuteketezwa.

Baada ya kupata taarifa hiyo ya operesheni, Mhe. Naibu Waziri aliweza kuongea na kuwahutubia wavuvi wa kijiji cha Kagongo, na baadae kufanya zoezi la kuteketeza nyavu haramu ambazo zilikamatwa kabla na wakati wa zoezi hili la operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu. Akiongea na wananchi hao alisema, wavuvi wanapaswa kulinda bwawa lao kwa manufaa ya vizazi vya baadae. Ameendelea kusema, anasikitishwa na kitendo cha kuona Supermarket zikiwa zinauza samaki kutoka nje ya nchi wakati, tuna uwezo mzuri wa kulinda na kuachana na uvuvi haramu. Amesema, uvuvi endelevu una manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na super market zetu kuuza samaki wetu wenyewe. Pia amesema, wavuvi wanapaswa kuthaminiwa, kwani nao wana mchango wa moja kwa moja kwenye katika kukuza uchumi wa nchi.

Mhe. Naibu Waziri hakuacha kutoa onyo kali kwa wale ambao bado wanaendelea na uvuvi haramu. Amesema, serikali haitakuwa na huruma na mtu yeyote anayevua kwa njia haramu ama mtu anayefadhili shughuli za uvuvi haramu na amesema kuwa, operesheni inayoendelea sasa ni endelevu. Pia amewataka wananchi wanaolima kandokando ya bwawa, kuacha shughuli hiyo mara moja. Amesema, kilimo kinachoendelea kandokando mwa bwawa, kinapelekea bwawa kupungua kina siku hadi siku.

Matangazo

  • Tangazo la kazi April 17, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira February 21, 2025
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA February 16, 2025
  • Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira January 30, 2025
  • Tazama Yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KARIBUNI TUMPOKEE MAKAMU WA RAIS – DC MWAIPAYA

    March 15, 2024
  • SERIKALI YAIPATIA SHULE YA MSINGI MWERO MILIONI 178.3

    October 12, 2023
  • MHE. TADAYO ATOA PONGEZI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO, ASEMA WILAYA INA VIONGOZI SAHIHI

    September 20, 2023
  • KIKUNDI CHA UTAMADUNI KUTOKA MWANGA KIMEULETEA MKOA WA KILIMANJARO USHINDI KWA AWAMU YA PILI MFULULIZO

    August 27, 2023
  • Tazama Yote

Video

Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATANGAZO
  • MIONGOZO
  • MFUMO WA USAJILI WA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI (PREM)
  • Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA)
  • Huduma za Afya
  • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Maktaba ya Picha
  • Kuomba kibali cha kusafiri nje ya nchi

Viunganishi Linganifu

  • PlanRep
  • Tovuti ya Ikulu
  • UTUMISHI
  • FFARs
  • Tovuti ya Wakala wa Serikali ya Mtandao
  • OR-TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga

    Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro

    Simu ya Mezani: +255 272974343

    Namba ya Simu: +255 272974343

    Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa