*Tanzania Utamaduni Carnival yaiteka Dar.*
Na John Mapepele
Matembezi ya Kiutamaduni yajulikanayo kama Tanzania Utamaduni Carnival yaliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yameliteka jiji la Dar es Salaam na kuandika historia hapa nchini.
Tanzania Utamaduni Carnival ni sehemu ya Tamasha la kitaifa la Utamaduni ambalo linazinduliwa alasiri ya leo Julai 2, 2022 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Tanzania Carnival imepita kuanzia uwanja wa Uhuru, daraja la Mfugale, daraja la Kijazi na daraja la Tanzanite.
Matembezi hayo ambayo yalipambwa na ngoma za makabila mbalimbali zimekuwa kivutio cha aina yake kwa wakazi wa Dar.
Mara baada ya kuwasili katika mtaa wa Kariakoo vikundi hivyo vilikaribishwa kwa mtindo wa aina yake hali iliyowafanya wananchi kujumuika kucheza kwa furaha nyimbo za makabila yao huku wakipongeza ubunifu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wa kuandaa tamasha na matembezi ya aina yake.
"Binafsi naipongeza Serikali kwa kutuandalia kitu kizuri na kikubwa kama hiki nashauri iendelezwe na kufanyika kila mwaka" amefafanua Isack Moga mfanyabiasha wa kariakoo.
Baadhi ya vivutio katika vikundi hivyo ni pamoja na kucheza na nyoka pia sarakasi za vijana waliokuwa wakiruka kutoka kwenye magari na kucheza kwa mtindo wa muziki wa kizazi kipya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa