Katika kuhakikisha Serikali inafanya kazi kwa kuwaletea maendeleo wananchi wake, Wilaya ya Mwanga kwa kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) imejipanga vilivyo kwa kuhakikisha barabara za mijini na vijijini zinafanyiwa ukarabati mzuri, sambamba na kuweka madaraja/karavati, mifereji na kutengeneza maeneo yaliyo korofi sanasana kipindi cha mvua.
Wilaya ya Mwanga kwa mwaka 2017/18 inakarabati barabara zake zilizoko kwenye tarafa zote tano za Wilaya ya Mwanga, ambazo ni Mwanga, Lembeni, Jipendea, Usangi na Ugweno kwa kutumia fedha zilizo tengwa kwa ajili ya barabara hizo.
Akieleza kiasi cha fedha kitakachotumika, kwa ukarabati wa barabara hizo, Ndugu Laurence Msemo ambaye ni Meneja wa TARURA wilayani Mwanga alisema kila tarafa imetengewa kiasi cha fedha kulingana na ukubwa wa kazi zinazo endelea. Tarafa ya Mwanga imetengewa kiasi cha Tsh. 244,710,000.00 kiasi ambacho, kitatumika kwenye ukarabati wa kawaida, kutengeneza sehemu korofi, kuweka makaravati, madaraja na mifereji. Tarafa za Usangi na Ugweno zimetengewa kiasi cha Tsh. 149,973,000 na tarafa za Lembeni na Jipendea nazo zikiwa zimetengewa kiasi cha Tsh. 215,590,022.40
Aidha Ndugu Msemo amesema kuwa pamoja na hali ya mvua inayoendela kwa sasa, na inayosababisha baadhi ya maeneo kazi kusimama, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi juni 2018 kazi za kutengeneza na kukarabati barabara hizo itakuwa imekamilika.
Kwa sasa maendeleo yanayo onekana kwenye barabara za mijini na vijijini kwa kiwango kikubwa yanachagwizwa na namna Serikali ilivyojipanga katika kuhakikisha inatimiza ahadi zake kwa wananchi na ndiyo maana kwa sasa serikali imeamua kuunda chombo maalum kitakachosimamia barabara zake za mijini na vijiji ambapo chombo hicho ni TARURA (Tanzania Rural Urban Roads Agency) ambapo kwa lugha ya Kiswahili wanafahamika kama Wakala wa Barara za Vijijini na Mijini.
Kwa kuliona hilo ni jukumu la kila mwananchi wa Wilaya ya Mwanga kuhakikisha anajivunia serikali yake iliyoko madarakani kwani kazi za maendeleo zinazofanywa zinamgusa mtu mmoja mmoja kwani huduma hizi zinawafikia hadi waliopo vijijini tena pasipo ubaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa