Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, imeweza kuvuka lengo lake la mwaka katika kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka 2022/2023, kwa kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 2.8 sawa na asilimia 112.
Hayo yamesemwa leo tarehe 17.08.2023 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Mhe. Dr. Salehe R. Mkwizu alipokuwa akitoa hotuba yake, kwenye mkutano wa mwaka wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mwanga.
Katika hotuba yake alisema kwamba, Halmashauri ya Mwanga imeendelea kusimamia na kukusanya vizuri mapato ya Halmashauri na ndio maana mapato yamekusanywa kwa zaidi ya asilimia 100. Nitumie fursa hii kuwapongeza Waheshimia Madiwani wangu, Mkurugenzi na timu ya wataalamu kwa kazi nzuri mliyo ifanya ya kuhakikisha kuwa, mapato yanakusanywa vizuri kwa maslahi mapana ya Halmashauri yetu, amesema Mhe. Mwenyekiti.
Sambamba na hayo, Mhe. Mwenyekiti amesema, kiasi cha Tsh. milioni 870, kiasi ambacho ni sehemu ya mapato ya Halmashauri kilipelekwa kwenye miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wa Mwanga.
Aidha, kupitia kikao hicho, Mheshimiwa Mwenyekiti alitumia fursa ya kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta kiasi kingi cha fedha, kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mwanga. Amesema kwamba, kwa mwaka 2022/2023 pekee, Wilaya ya Mwanga imeweza kupokea kiasi cha Bilioni 12.5, fedha ambazo zimetumika katika kuendeleza miradi ya afya, utawala na elimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, leo imefanya mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri kwa ajili ya kupitia taarifa ya utendaji na uwajibikaji ya Halmashauri kwa mwaka 2022/2023.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa