Uvuvi katika Bwawa la nyumba ya Mungu wasimamishwa kwa kipindi cha Miezi sita ili kuongeza uzalishaji na ukuaji wa samaki. Utaratibu huu wa kufunga bwawa kwa miezi sita na kufunguliwa baada ya miezi sita ni endelevu na ni makubaliano kati ya Wakuu wa Mikoa Miwili ambayo ni Mkoa wa Kililimanjaro na Manyara ambayo inapakana na bwawa hili. Wakazi waliozunguka Bwawa hilo ambao wengi wao ni Wavuvi wanashauriwa kujihusisha na kazi mbadala na kutotegemea uvuvi tu. Bwawa hilo limefungwa na kusimamisha shughuli za uvuvi kuanzia tarehe 4/1/2018 na viongozi wa Mkoa na Halmashauri husika, likiambatanisha na zoezi la uchomaji wa nyavu haramu zinazotumiwa na wavuvi wasio waaminifu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa