Vijana wa Wilaya ya Mwanga wameaswa kufuata na kudumisha maadili na Utamaduni wa Mtanzania kwa kuhakikisha kwamba, wanakemea mila na desturi zisizofaa katika jamii na katika maisha yao ya ujana ya kila siku.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Ndg. Eliakimu E. Kimuto, aliyekuwa Mgeni Rasmi kwenye fainali ya kombe la pasaka lililo andaliwa na mdau wa michezo Ndg. Raymond Kyarua Abraham wa Mwanga.
Ndg. Kimuto amesema kwamba, vijana wanapaswa kukemea kwa nguvu zote, matendo maovu ambayo yamekuwa yakiibuka kwenye jamii zetu ikiwa ni matendo yaliyo kinyume na maadili ya mtanzania. Ameendelea kueleza kwamba, kwa sasa suala la ushoga linapaswa kukemewa kwa mbinu zote, huku vijana wakipaswa kuwa mstari wa mbele katika kukemea mambo ya ushoga. "Haipendezi wazazi wetu wakawaona vijana wao wakiiga tamaduni zisizo faa, kwani wakiwa kama wazazi wanaumia pale wanapo waona vijana wao wakiwa katika mwenendo usiofaa, amesema Ndg. Kimuto.
Sambamba na hayo, amewaasa jamii ya wana Mwanga, kuhakisha wanaupenda utamaduni waliolelewa nao, utamaduni ambao unaenzi tunu za taifa letu la Tanzania.
Naye mdau wa michezo Ndg. Raymond Kyarua Abraham, ambaye ndiye aliye andaa ligi hiyo ya pasaka Wilayani Mwanga, amewapongeza vijana walioweza kushiriki ligi ya Pasaka kwa kusema kwamba, michezo inaimarisha urafiki, inajenga umoja pamoja na kuimarisha afya ya mwili na akili.
Ligi hiyo ya Pasaka ilizishirikisha timu tano, ambazo ni Wakongwe FC, Reli Juu, Bodaboda, TRA na Jitimai. Timu zilifanikiwa kuingia fainali ni Wakongwe FC na Reli Juu, ambapo timu ya Wakongwe waliibuka washindi wa ligi hiyo kwa kuwafunga Reli Juu kwa mabao matano ya penati dhidi ya mabao matatu ya Reli Juu.
Ndg. Raymond amewaasa wadau mbalimbali wa michezo wa ndani na nje ya Wilaya ya Mwanga kuwekeza kwenye michezo kwa kusema kwamba, wadau wakijitokeza watawasaidia vijana wengi kutojihusisha na matendo maovu kama ngono uzembe, ambapo inaweza kupelekea kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa